Kwa mujibu wa Ofisi ya Mahusiano ya Umma ya Shirika la Wanazuoni wa Qur'ani Iran, linalofanya kazi chini ya Akademia ya Elimu, Utamaduni na Utafiti ya Iran (ACECR) , maandalizi yanaendelea kwa mashindano haya ya saba ya kimataifa. Juhudi hizi ni mwendelezo wa miaka 39 ya harakati za Qur'ani zinazofanywa na ACECR kwa msaada wa wanazuoni na wanaharakati waliobobea katika uwanja huu.
Toleo la mwaka huu linafuatia mafanikio ya mashindano sita yaliyopita, ambayo yamepokea washiriki kutoka zaidi ya nchi 85 na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuhamasisha utamaduni wa Qur’ani na mwelekeo wa Kiislamu duniani kote.
Hatua ya awali ya mashindano ilifanyika kwa njia ya mtandao kupitia majukwaa ya kidijitali mwezi Machi mwaka huu. Katika muktadha huu, uratibu ulifanyika katika balozi mbalimbali za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ili kuteua wanafunzi watakaowakilisha nchi zao katika makundi mawili: usomaji wa Qur’ani na hifdh ya Qur’ani yote, ambapo ushiriki uliboreshwa mahsusi kwa wanafunzi wa kiume wa vyuo vikuu.
Kwa mara ya kwanza katika mashindano haya, sehemu maalum ya “Teknolojia na Ubunifu Kuhus Qur’ani” imetangazwa, ikilenga wanazuoni wa vyuo vikuu kutoka ulimwengu wa Kiislamu. Washindi wa kundi hili watatuzwa ana kwa ana katika hatua ya mwisho ya mashindano hayo.
Tukio hili lenye hadhi kubwa linatoa fursa adhimu ya kuendeleza utamaduni wa Qur’ani miongoni mwa wanafunzi wa Kiislamu wa vyuo vikuu duniani kote, likichochea ushirikiano wa kielimu na kiutamaduni.
Wakati tarehe ya mwisho ya usajili kwa makundi ya hifdh na usomaji wa Qur’ani ilimalizika Februari 28, 2025, tarehe ya mwisho kwa sehemu ya Teknolojia na Ubunifu Kuhusu Qur’ani ni Aprili 20, 2025.
3491922