IQNA

Makabiliano na Mabeberu

Jeshi la Wanamaji la Iran lainasa meli ya mafuta ya Marekani kufuatia agizo la mahakama

22:31 - January 11, 2024
Habari ID: 3478185
IQNA- Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limetangaza kuikamata meli ya mafuta ya Marekani kwa amri ya mahakama katika Bahari ya Oman.

Kufuatia kukamatwa meli ya Suez Rajan, Mei mwaka jana, na wizi wa mafuta ya Iran uliofanywa na Marekani kwenye meli hiyo, meli ya mafuta yenye jina jipya St Nicholas imekamatwa katika maji ya Bahari ya Oman mapema leo Alhamisi.

Meli ya mafuta ya Iran iliyokuwa na bendera ya Visiwa vya Marshall, Suez Rajan, ilikamatwa kinyume cha sheria na Washington mwezi Aprili 2023 kwa kisingizio cha "operesheni ya kutekeleza vikwazo" na kupelekwa kwenye bandari ya Texas.

Meli hiyo ya mafuta, iliyopewa jina jipya la ST Nicholas, ilikuwa imebeba mafuta katika Bahari ya Oman, na imetekwa na jeshi la kistratijia la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa amri ya mahakama na idhini ya Shirika la Bandari na Meli, kulipiza kisasi cha wizi wa mafuta uliofanywa na Marekani na inasafirishwa kuelekea kwenye bandari za Jamhuri ya Kiislamu ambako itakabidhiwa kwa mamlaka ya mahakama.

Awali, Shirika la Operesheni za Biashara ya Baharini la Uingereza (UKMTO) lilitangaza kuwa meli ya mafuta yenye bendera ya Visiwa vya Marshall, St Nicholas, ilipakiwa mafuta mwendo wa saa 7:30 (0330 GMT) kutoka Sohar nchini Oman na kwamba imebadili mwelekeo kuelekea Bandar-e-Jask nchini Iran.

Marekani imekuwa ikitumia mabavu kutwaa meli zinazopakia mafuta za Iran na nchi nyingine katika maji ya kimataifa na kuiba bidhaa hiyo. 

4193418

captcha