IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Washindi wa mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya wanafunzi Iran watangazwa

14:03 - February 22, 2024
Habari ID: 3478395
IQNA - Kamati ya maandalizi ya mashindano ya 8 ya kimataifa ya Qur'ani kwa wanafunzi wa shule imetangaza washindi.

Mashindano hayo yaliandaliwa kwa pamoja na Wizara ya Elimu ya Iran na Shirika la Wakfu na Misaada la Iran wiki hii, sambamba na Awamu ya 40 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran.

Washindani walishindana katika kategoria za usomaji na kuhifadhi Qur'ani nzima katika sehemu mbili tofauti za wasichana na wavulana.

Kwa mujibu wa jopo la majaji, Mohanna Qanbari Shirzili kutoka Iran amechukua nafasi ya kwanza katika kategoria ya kuhifadhi Qur'ani Tukufu katika sehemu ya wasichana.

Diyatara Andia Busu kutoka Senegal na Maimanua Munir az-Zaman kutoka Bangladesh wameibuka wa pili na wa tatu mtawalia.

Asma Falaki, mshindi wa juu katika usomaji wa usomaji wa wasichana, pia anatoka nchi mwenyeji huku Reyhaneh Moghaddas kutoka Afghanistan na Zahra Taghi al-Matlashi kutoka Iraq akishika nafasi ya pili na ya tatu.

Katika sehemu ya wavulana, Mehdi Akbari Zarin wa Iran aliibuka wa kwanza. Mshindi wa pili amekuwa ni Muhammad Abu Bakr kutoka Pakistan na mshindi wa tatu ni Mushfiq Rahman kutoka Bangladesh.

Mshindi mkuu katika kuhifadhi Quran nzima ni mwanafunzi wa Bangladesh Ahmad Bashir, Seyed Mohammad Sadeq Hosseini kutoka Iran amekuwa wa pili na Abdullahi Abdullahi Giray kutoka Nigeria ndiye mshindi wa daraja la tatu.

Baada ya awamu ya awali, jumla ya wanafunzi 30 kutoka nchi 15 walifuzu kwa awamu ya mwisho ya shindano hilo.

Walioingia fainali walikuwa kutoka Afghanistan, Indonesia, Uganda, Bangladesh, Pakistan, Uturuki, Tunisia, Senegal, Iraq, Iran, Oman, Gambia, Malaysia, Nigeria, na New Zealand.

4201104

captcha