IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Siku ya Kwanza ya Mashindano ya 40 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran

11:36 - February 17, 2024
Habari ID: 3478365
IQNA - Ijumaa ilikuwa siku ya kwanza ya Awamu ya 40 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran yanayofanyika mjini Tehran ambapo kulikuwa na washiriki 13 walipanda jukwani.

Wasomaji na wahifadhi Qur'ani wanne wa kiume walipanda jukwaani ikiwa ni sehemu ya toleo la 8 la mashindano ya kimataifa ya Qur'ani kwa wanafunzi wa shule za Kiislamu duniani yanayofanyika sanjari na Awamu ya 40 ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran.

Katika kategoria za watu wazima za usomaji wa Tarteel na Tahqiq, wawakilishi wa kiume kutoka Iran, Iraq, Uingereza, Algeria, Russia, Indonesia, Misri, India, na Ujerumani walipanda jukwaani.

Usomaji wao unaweza kutazamwa kupitia kiunga hiki.

Mashindano hayo pia yalishirikisha vipindi mbalimbali vya kitamaduni na kisanii pembeni, kama vile qasida ya vijana 164 wa Kiirani ambayo iliwavutia watazamaji na majaji.

Mashindano ya 40 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yalianza Alkhamisi mjini Tehran katika sherehe iliyohudhuriwa viongozi wa Iran na wapenda Qur'ani kutoka sehemu mbalimbali za dunia.

Kwa mujibu wa waandaaji hao, zaidi ya wawakilishi wa nchi 110 walijiandikisha kushiriki mashindano hayo na walioingia fainali ni washiriki 69 kutoka nchi 40 zilifuzu kwa awamu ya mwisho baada ya mchujo wa awali.

Mashindano hayo yanatazamiwa kuendelea hadi Jumanne, Februari 20, na washindi watatangazwa na kutunukiwa katika hafla ya kufunga Jumatano, Februari 21.

Washiriki wanashindania zawadi za juu katika kategoria za usomaji wa Qur'ani (kwa wanaume) na kuhifadhi Qur'ani na usomaji wa Tarteel (kwa wanaume na wanawake).

Hafla hiyo ya kila mwaka inayoandaliwa na Jumuiya ya Masuala ya Wakfu na Misaada, inalenga kukuza utamaduni na maadili ya Qur'ani miongoni mwa Waislamu na kuonyesha vipaji vya wasomaji na wahifadhi Qur'ani.

 

4200198

Habari zinazohusiana
captcha