IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Kauli mbiu ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran inahusu matukio ya kikanda

14:16 - February 17, 2024
Habari ID: 3478366
TEHRAN (IQNA) - Kauli mbiu ya Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran mwaka huu imechaguliwa kutokana na matukio ya kieneo na mauaji yanayoendelea ya Wapalestina huko Gaza, afisa mmoja alisema.

Fainali ya Mashindano ya 40 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran ilianza Alhamisi mjini Tehran kwa kauli mbiu ya "Kitabu Kimoja, Umma Mmoja, Kitabu cha Muqawama (Mapambano ya Kiislamu)".

Akizungumza katika mahojiano ya televisheni siku ya Ijumaa, Mkuu wa Shirika la Masuala ya Wakfu na Misaada la Iran, ambalo limeandaa mashindano hayo, Hujjatul Islam Seyed Mehdi Khamoushi alisema kauli mbiu hiyo inahusiana na matukio ya kieneo, ikiwa ni pamoja na Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa iliyoanzishwa na harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas na hujuma za utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza.

Imekuwa ni jambo la kawaida  kwamba kauli mbiu ya tukio hili kuu la Qur'ani huchaguliwa kila mwaka kulingana na maendeleo au matukio katika ulimwengu wa Kiislamu, alibainisha.

Motto of Iran’s Int’l Quran Contest Related to Regional Developments: Official

Mawanazuoni  huyo ameongeza kuwa, lau nchi zote za Kiislamu zingetekeleza wajibu wao ipasavyo katika kukabiliana na mstari wa mbele wa Kufr, ambao mfano wake mkubwa ni utawala wa Kizayuni, ulimwengu wa Kiislamu haungeshuhudia maafa hayo huko Gaza.

Kwingineko katika maelezo yake, Hujjatul Islam Khamoushi alibainisha kuwa baada ya duru ya awali iliyofanyika kwa kushirikisha nchi 110, wawakilishi kutoka nchi 44 wamefuzu kwa fainali hizo na wanachuana katika makundi ya usomaji na kuhifadhi Qur'ani. Quran nzima.

Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni hafla ya kila mwaka ambayo huwavutia wasomaji na wahifadhi Qur'ani kutoka sehemu mbalimbali za dunia.

Hulenga kukuza utamaduni na maadili ya Qur'ani, na pia kukuza urafiki na ushirikiano kati ya nchi za Kiislamu.

4200189

Habari zinazohusiana
captcha