IQNA

Mwokozi

Ahadi yenye bishara njema katika Qur'ani Tukufu

18:48 - February 28, 2024
Habari ID: 3478429
IQNA – Qur’ani Tukufu inatoa bishara kwamba itakuja zama ambapo Uislamu utatawala dunia nzima na Waislamu watatekeleza mafundisho yao ya kidini bila ya woga wowote.

Qur'ani Tukufu inatoa habari njema juu ya watu wema kurithi ardhi kama ahadi ya Mwenyezi Mungu kwa waumini:

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” (Aya ya 55 ya Surah An-Nur)

Aya hii inaahidi kwamba waumini wanaotenda mema wataunda jamii ambayo ina sifa fulani. Kwanza, wanairithi ardhi kama wale waliokuwa kabla yao waliokuwa na madaraka. Kurithi kwao ardhi  kunategemea kukusanya kwao watu wema. Hao ndio watu wema na wanapigania mema.

Pili, Dini yao itasimama duniani na kutofautiana kwao katika kanuni na uzembe wao katika kutekeleza sheria ndogondogo hakutaitikisa dini yao na unafiki hautawaathiri. Wakati huo, Waislamu hawatakuwa katika mfumo wa madhehebu mengi kama ilivyo sasa ambapo baadhi huwachukulia wengine kuwa ni makafiri.

Tatu, hofu itageuka kuwa usalama ili wasiwe na khofu juu ya dini au maadui wa ndani au wa nje.

Hivyo kwa ujumla, ahadi tatu kuhusu jamii hii ni kurithi na kuitawala ardhi, kueneza dini yao duniani na kuondoa vyanzo vyote vya ukosefu wa usalama.

Ahadi hizi adhimu ambazo zimesisitizwa katika aya hii bado hazijatekelezwa. Ni lini watu waadilifu wameweza kutawala duniani kote kwa rehema na uadilifu wao na kuweka kanuni zao kwa uhuru kamili na bila woga? Hivyo basi, kama ahadi hii ya Qur'ani Tukufu itatimizwa, itakuwa wakati wa Mwokozi aliyeahidiwa. Na Hadithi Mutawatir kutoka kwa Mtukufu Mtume (SAW) zinaashiria ukweli kwamba jamii kama hiyo itakuja.

3487331

Kishikizo: mwokozi
captcha