IQNA

Mwokozi

Usomaji wa Aya za Qur’ani Tukufu kuhusu kudhihiri Mwokozi (+Video)

17:29 - February 25, 2024
Habari ID: 3478410
IQNA - Mashindano ya 40 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran yamekamilika mapema wiki hii, siku chache kabla ya Nisf-Shaaban, ambayo inaadhimisha kuzaliwa kwa Imam Mahdi (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake).

Katika hafla hii adhimu, IQNA iliwataka baadhi ya wajumbe wa jopo la majaji na washindani katika tukio hilo la kimataifa la Qur'ani kusoma aya mbili za Qur'ani zinazohusu ujio wa Mwokozi mwishoni mwa zama:

Aya ya 5 ya Surat Al-Qasas: “Na tukataka kuwafadhili walio dhoofishwa katika nchi hiyo na kuwafanya wawe waongozi na kuwafanya ni warithi.”

Amirul-Mu’minin (AS) alisema katika tafsiri ya aya hii: “Dunia itainama kuelekea kwetu baada ya kuwa kinzani kama ngamia jike anayepata lishe akiwa anaelekea kwa makinda wake.

Kisha akasoma Aya ya 5 ya Sura Al-Qasas.

Kwa mujibu wa Ibn Abi al-Hadid, wanazuoni wa kidini wanaamini kwamba kauli hii ya Imam Ali (AS) inaonyesha Imamu mkubwa na kiongozi atakuja ambaye atatawala ardhi na nchi zote zitakuwa chini ya usimamizi wake.

Imepokewa pia kwamba Imam Ali (AS) alisema kwamba Nyumba ya Mtukufu Mtume (SAW) ndio ambayo Quran inasema watafanywa Maimamu na warithi.

Aya ya 105 ya Surah Al-Anbiya: “Tumeandika katika Zaburi tulizoziteremsha baada ya Taurati kwamba ardhi watapewa waja wetu wema kama urithi wao.

Imam Baqir (AS) alisema katika tafsiri ya aya hii kwamba waja wema wa Mwenyezi Mungu waliotajwa katika aya hii ni Imam Mahdi (AS) na masahaba zake mwishoni mwa zama.

Mashindano ya 40 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran yalifanyika Tehran tarehe 18-24 Februari yakiwa na kauli mbiu ya "Kitabu Kimoja, Umma Mmoja, Kitabu cha Muqawama".

Baadhi ya washiriki katika mashindano wakisoma aya hizo mbili:

Baadhi ya majaji wakisoma aya hizo mbili :

3487325

 

Kishikizo: mwokozi imam mahdi
captcha