IQNA

Dunia kamwe haitbaki bila Uongozi wa Mwenyezi Mungu

22:27 - February 23, 2024
Habari ID: 3478404
IQNA – Imepokewa kutoka katika Aya ya 7 ya Surah Ar-Raad kwamba siku zote kuna uongozi wa kiongozi aliyechaguliwa na Mwenyezi Mungu katika jamii za wanadamu na hivyo ardhi haijawahi kukosa mtu ambaye ni Hujjat (ushahidi au hoja ya Mwenyezi Mungu).

Ujio au kudhihiri mwokozi ambaye atakuja kuujaza ulimwengu haki ni imani iliyooenea katika aghalabu ya dini na imani. Kuna tofauti za maoni kuhusu mwokozi ni nani na kuhusu baadhi ya sifa zake.

Katika Qur’ani Tukufu, kuna makundi mawili ya aya ambazo mtu anaweza kukisia suala la ujio wa mwokozi. Kundi la kwanza linajumuisha aya zinazoelezea uwepo wa Hujjat (ushahidi  au hoja ya Mwenyezi Mungu) miongoni mwa watu kama inavyohitajika. Kundi la pili ni la aya zinazotoa bishara ay habari njema kwamba waadilifu na waliokandamizwa watatawala dunia katika mustakabali. Hapa ni baadhi ya pointi kuhusu kundi la kwanza:

Quran Tukufu inasema katika Aya ya 7 ya Surah Ar-Raad: “(Muhammad), Hakika wewe ni Mwonyaji, na kila kaumu ina wa kuwaongoa.

Imekisiwa kutokana na Aya hii kwamba kuna aina mbili za walinganiaji kwenye haki: Mwenye kuonya na anayeongoza. Kuna tofauti gani kati ya hizo mbili? Mwonyaji ni kwa ajili ya kuwasaidia waliopotoka kurejea katika njia iliyonyooka ambapo mwongozo ni kwa ajili ya kuwasaidia wale walio katika njia iliyo sawa ili kusonga mbele.

Hapana shaka kwamba ndani ya aya hizo, Mtume (SAW) ameelezwa kuwa ni mwonyaji lakini kinachoeleweka kutokana na aya hii ni kwamba muongozo hapa utabainishwa asiyekuwa Mtume (SAW), ambaye ataendeleza njia yake na kuilinda dini yake.

Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 24 ya Surah Al-Fatir: “Na hapana umma wowote ila ulipata mwonyaji kati yao.”

Kwa hiyo kwa mujibu wa Aya ya 24 ya Surah Al-Fatir, kumekuwepo Nabii wa Mwenyezi Mungu katika kila umma kuwa ni mwonyaji na kwa mujibu wa Aya ya 7 ya Surah Ar-Raad, kuna muongozaji katika kila umma.

Wanachuoni wengi mashuhuri wa Kisunni kama Ibn Kathir, Tabari, Fakhr Razi, Abu Hayyan Andulusi na Neyshaburi wamenukuu riwaya kutoka kwa Ibn Abbas katika kufasiri sentensi hii: Mtukufu Mtume (SAW) aliweka mkono wake juu ya kifua chake na akasema: “Mimi ndiye muonyaji” kisha akaashiria kwenye bega la Ali (AS) na kusema: “Wewe ni kiongozi na baada yangu utawaongoza walioongoka!”

Kwa hiyo inakisiwa kutokana na aya hii kwamba daima kuna mwongozaji katika jamii za wanadamu ambao wamechaguliwa na Mwenyezi Mungu. Katika historia yote ya wanadamu, dunia haijawahi kuwa na haitabaki bila kiongozi na Hujjat mwenye sifa hizo za muongozaji.

3487245

Kishikizo: mwokozi imam mahdi
captcha