IQNA

Mafuriko Saudia

Mafuriko ya ghafla katika mji mtakatifu wa Makka (+ Video)

21:22 - December 23, 2022
Habari ID: 3476292
TEHRAN (IQNA)- Mafuriko makubwa yalikumba mji mtakatifu wa Makka nchini Saudi Arabia siku ya Ijumaa asubuhi kufuatia mvua kubwa iliyonyesha usiku, kuharibu magari na mali katika mji huo.

Picha za video za mafuriko hayo zinaonyesha magari yakisombwa na mafuriko ya maji, huku barabara kuu kadhaa zikifungwa.

Mji wa Makka ulishuhudia mvua kubwa Alhamisi usiku hadi Ijumaa asubuhi. Kituo cha Kitaifa cha Utabiri wa Hali ya Hewa kilitoa onyo la hali ya hewa katika jimbo la Makka siku ya Ijumaa huku mvua ikiendelea kunyesha kwa viwango vya wastani hadi muhimu katika maeneo ya Rania, Taif, Adham na Maysan.

Picha za video kutoka Msikiti Mkuu wa Makka zilionyesha mvua ikinyesha huku waumini wakiwa wanaendelea na ibada ya Hija ndogo ya Umrah.

Uwanja wa ndege wa Mfalme  Abdulaziz mjini Jeddah uliwaomba wasafiri wapige simu ili kuthibitisha hali ya safari zao za ndege kabla ya kuelekea uwanja wa ndege, kwani baadhi ya safari za ndege zilitarajiwa kusitishwa kutokana na hali mbaya ya hewa.

Kituo cha utabiri wa hali ya hewa pia kilionya kuhusu mafuriko na ngurumo zinazoambatana na mvua kubwa katika mkoa wa Jeddah ulio kaskazini mwa Makka.

Mnamo Novemba, watu wawili walikufa katika mafuriko ambayo yalikumba mji wa pwani wa Jeddah kutokana na mvua kubwa ambazo hazijawahi kushuhudiw akwa muda mrefu mjini humo.

3481792

captcha