IQNA

Turathi za Kiislamu

Msikiti wa Shajarah nje ya Madina

IQNA – Msikiti wa Shajarah, unaojulikana pia kama Msikiti wa Dhul Hulaifah na Al-Ihram, ni miongoni mwa misikiti ya kihistoria katika mji mtakatifu wa Madina.

Uko kilomita 8 nje ya Madina katika eneo la Dhul Hulaifah kwenye njia ya kuelekea Makka. Eneo hilo ni Miqat kwa wale wanaotoka Madina kwenda Makka kwa ajili ya Hija au Umrah.

Miqat ni mpaka mkuu ambao wanaokusudia kushiriki ibada ya Hija au Hija ndogo ya Umrah lazima waingie katika hali ya Ihram (wawe Muhrim). Baada ya kutembelea Msikiti wa Mtume huko Madina, waumini  huenda kwenye Msikiti wa Shajareh ili kuwa Muhrim.

Mtu anaweza tu kuwa Muhrim baada ya kuusafisha mwili, kuvaa mavazi maalumu na kufanya Niyyah kabla ya Miqat iliyowekwa. Matendo fulani, kama vile kukata nywele au kupaka manukato, ni haramu kwa Muhrim.

 
Kishikizo: hija