IQNA

Hija katika Qur'ani /1

Watu wenye uwezo wanawajibika mbele ya Mwenyezi Mungu kuhusu Hija

15:44 - May 21, 2025
Habari ID: 3480719
IQNA – Qur'ani Tukufu inaitazama Hija kama haki ya Mwenyezi Mungu juu ya wanadamu, na ni wajibu kwa wale wote walio na uwezo wa kufika katika Nyumba ya Mwenyezi Mungu katika mji mtakatifu wa Makka.

Wajibu huu si ibada tu, bali pia unachukuliwa kama ishara ya imani ya kweli.

Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 97 ya Surah Aal-Imran:
“*Ndani yake zipo Ishara zilizo wazi - masimamio ya Ibrahim, na mwenye kuingia humo anakuwa katika amani. Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia ya kwendea. Na atakaye kanusha basi Mwenyezi Mungu si mhitaji kwa walimwengu.”

Aya hii inaonesha kuwa kutekeleza ibada ya Hija ni wajibu ambao Mwenyezi Mungu amewajibisha wale walio na uwezo. Neno "Istitaa’a" (uwezo) katika aya hii halimaanishi uwezo wa kifedha pekee, bali pia linajumuisha uwezo wa kimwili, usalama wa safari, hali ya kiafya, na uwezo wa kuendesha maisha baada ya kurejea.

Muendelezo wa aya unaosema: “Na atakayekufuru, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mkwasi…” unatufundisha kuwa kuacha Hija kwa makusudi ni aina ya ukafiri na dharau kwa amri ya Mwenyezi Mungu.

Katika aya hii ya Hija, kuacha kuhiji kumetajwa kama kufr (ukafiri). Baadhi ya wafasiri wanaona kufr hii kuwa ni kuritadi au kuasi dini, yaani mtu anayekataa kwamba Hija ni wajibu huondoka kwenye Uislamu. Hata hivyo, wapo wanaoamini kuwa kuacha Hija – hata bila kukataa kuwa ni wajibu – kunaweza kuchukuliwa kama kutoka katika mipaka ya Uislamu. Pia, kuna wale wanaoelewa kuwa neno kufr linaweza kumaanisha upinzani wowote dhidi ya ukweli, ingawa lina viwango tofauti na kila kiwango kina hukumu zake maalum.

Kutokana na mtazamo wa baadhi ya wafasiri, usemi "Ayat Bayyinat" (ishara zilizo wazi) unarejelea dalili dhahiri za Nyumba ya Mwenyezi Mungu, na pamoja na aya iliyotangulia, inakuwa ni jibu kwa Wayahudi waliokuwa wakiheshimu zaidi mji wa Jerusalem (al-Quds) kuliko Kaaba.

Kama jibu kwa upinzani wa Wayahudi, Qur'ani inaangazia fadhila maalum za Kaaba katika aya iliyotangulia, na katika aya hii inaongeza “ishara zilizo wazi”.

Kwa mujibu wa aya ya Hija, mambo yanayoonekana kama ishara wazi za Nyumba ya Mwenyezi Mungu ni pamoja na Maqam Ibrahim (mahali aliposimama Ibrahim), usalama anaoupata aingiaye humo, na wajibu wa Hija kwa wale wote walio na uwezo.

3493180

Habari zinazohusiana
Kishikizo: hija qurani tukufu
captcha