Kama ilivyoripotiwa na Kurugenzi Kuu ya Pasipoti (Jawazat), kufikia mwisho wa Jumapili, jumla ya idadi ya Waislamu walioingia kwenye Ufalme kupitia anga, nchi kavu, na bandari za baharini kwa ajili ya Hija ilifikia 935,966.
Takribani, 896,287, walisafiri kwa ndege, wakati 37,280 walifika kwa njia ya nchi kavu, na 2,399 waliingia kupitia bandari za bahari, kulingana na takwimu za Shirika la Habari la Saudi.
Jawazat imeeleza dhamira yake ya kurahisisha mchakato wa kuingia kwa waumini wanaofika nchini humo kwa ajili ya Hija, na kuimarisha majukwaa yake ya mtandaoni katika bandari zote za kimataifa kwa vifaa vya hali ya juu vya kiufundi. Kwa ujumla mwaka huu waumini karibu milioni mbili wanatarajiwa kushiriki katika ibada ya Hija.
Hija, ni ibada ya faradhi ibada ya lazima kwa Waislamu wanaokidhi vigezo vya kimwili na kifedha, inatarajiwa kutimizwa angalau mara moja katika maisha yao.
3488616