Shirika la Habari la Saudia (SPA) lilimnukuu Waziri wa Afya,Fahad bin Abdul-Rahman Al-Jalajel, akisema kwamba: "Idadi ya vifo ilifikia 1,301, na 83% kati yao hawakuwa na vibali vya kuhiji ambao walitembea masafa marefu chini ya miale ya jua, bila mahali pa kujikinga wala kupumzika.”
Al-Jalajel ameongeza kuwa, hakuna magonjwa ya mlipuko au ya kuambukiza yaliyorekodiwa, akisisitiza kuwa mfumo wa afya umetoa huduma za matibabu maalumu zaidi ya 465,000 kwa mahujaji.
Msimu wa Hija mwaka huu ulisadifiana na hali ya hewa ya joto kali, kiasi kwamba halijoto ilifikia nyuzi joto 51.8 kwenye kivuli mjini Makka wakati wa ibada ya Hija.
Wakati huo huo Waziri wa Hija wa Saudi Arabiaa, Tawfiq Al-Rabiah, ametangaza kuwa idadi ya mahujaji mwaka huu wa 1445 Hijria ilifikia 2,833,164 kutoka zaidi ya nchi 200, wakiwemo wahujaji 221,854 kutoka ndani ya Saudi Arabia.
3488868