Hija ambayo ni moja ya mikusanyiko mikubwa zaidi ya kidini ulimwenguni mwaka huu imerejea katika uwezo wake kamili kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa janga la coronamiaka mitatu iliyopita.
Hija ni moja ya nguzo tano za Uislamu, na Waislamu wote wenye uwezo wa kimwili na kimali wanatakiwa kuhiji angalau mara moja katika maisha yao.
Saudi Arabia imetangaza kuwa, siku ya kwanza ya mwezi wa Dhul-Hijjah ilikuwa Juni 7, na hivyo Jumamosi, Juni 15 itakuwa siku ya Arafah, na Jumapili Idul al-Adha.
Tangazo hili liliungwa mkono na mamlaka za kidini za Misri, Jordan, Palestina, UAE, Tunisia, Algeria, na Libya.
Kwingineko Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Indonesia, Malaysia, Brunei, India na Oman pamoja na nchi kadhaa za Afrika zikiwemo Morocco, Mauritani zimetangaza kuwa, kwa kutegemea mwandamo wa mwezi, Jumatatu, Juni 17 itakuwa ni siku kuu ya Idul Adha.
Ofisi ya Ayatullah Seyyed Ali Sistani nchini Iraq nayo imetangaza kuwa Jumamosi ilikuwa ya kwanza ya mwezi wa Dhul-Hijjah, 1445 Hijria, na hivyo Idul Adha itakuwa tarehe 17 Juni.
3488703