IQNA

Msafara wa Qur'ani wa Nur kutoka Iran kushiriki vikao 220 vya Qur'ani wakati wa Hija

17:18 - May 13, 2025
Habari ID: 3480682
IQNA – Msafara wa Qur'ani wa Nur (Noor) kutoka Iran, ambao ni ujumbe wa wasomaji Qur'ani, unajiandaa kuendesha zaidi ya matukio 220 ya Qur'ani wakati wa ibada ya Hija ya mwaka huu wa 1446 Hijria (2025) katika miji mitakatifu ya Makka na Madina.

Msafara wa Qur'ani wa Nur kutoka Iran kushiriki vikao 220 vya Qur'ani wakati wa HijaAkizungumza na IQNA, Mohammad-Javad Kashefi—msomaji wa kimataifa wa Qur'ani na kiongozi rasmi wa msafara huo—alisema kuwa timu hiyo ina jumla ya wanachama 20, wakiwemo wasomaji 14 wa Qur'ani (qari), hafid mmoja wa Qur'ani, na kikundi cha watu watano cha Tawasheeh (waimbaji wa kaswida na nyimbo za Kiislamu).

“Wanachama hawa wamegawanywa katika makundi tofauti na watasafiri kwa awamu,” alisema. “Wasomaji wengi wa Qur'ani katika kundi hili ni maarufu kitaifa na kimataifa. Licha ya uzoefu wao mkubwa, kikosi cha mwaka huu kinajumuisha kizazi kipya, chenye wastani wa umri wa miaka 32.”

Kashefi alisisitiza kuwa ujumbe huo umejiandaa kikamilifu kwa ajili ya kuwa na vikao vya  hali ya juu kiroho na kitaaluma wakati wa ibada hiyo ya Hija.

“Tunatarajia kuwa qira’a zitakazotolewa na kundi hili zitakuwa na athari kubwa ya kiroho kwa hadhira,” aliongeza.

Msafara wa Nur ni sehemu ya juhudi pana za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuboresha upeo wa kiroho na kimaanawi wa Mahujaji  kwa kuandaa matukio ya Qur'ani katika kipindi chote cha Hija. Kila mwaka, mamilioni ya Waislamu kutoka kona mbalimbali za dunia hukusanyika mjini Makka kwa ajili ya ibada hii tukufu, na Iran hupeleka pia wanaharakati wa Qurani pamoja na mahujaji wake.

Iran’s Noor Quranic Convoy to Hold Over 200 Quranic Programs During 2025 Hajj

Kashefi alibainisha kuwa vikao vya Qur'ani vilivyopangwa vitafanyika katika miji yote miwili—Makka na Madina. “Tunatarajia kuwa kutakuwa na takriban mikusanyiko 220 ya qira’a,” alisema. Ingawa vipindi vingi tayari vimepangwa, aliongeza kuwa “asilimia kama 30 ya matukio yatategemea hali halisi ya siku husika na yataamuliwa papo hapo.” Kuhusu msimamo wa msafara huo juu ya masuala yanayoendelea katika Ulimwengu wa Kiislamu, hasa kuhusu Gaza na Palestina, Kashefi alisema: “Tutajitahidi kuchukua nafasi yenye maana. Kabla na baada ya kila qira’a, tutawasilisha aya za Qurani zinazowataka Waislamu kusimama dhidi ya dhulma na kutetea haki za wanyonge.”Aliongeza kuwa:“Qurani ni lugha ya pamoja ya Waislamu wote, na tunapaswa kuitumia kama mwongozo wa kuongeza uelewa kuhusu kile kinachoendelea Gaza na Palestina.”

3493069

Habari zinazohusiana
Kishikizo: hija msafara wa nur
captcha