IQNA

Vidokezo vya Afya kwa Mahujaji: Jinsi ya kuepuka mafua ya kawaida

17:22 - June 05, 2024
Habari ID: 3478936
IQNA - Mtaalamu wa afya ametoa mapendekezo ya kuzuia homa au mafua ya kawaida wakati wa msimu Hija.

Wakati wa Hija, mahujaji mara nyingi hukabiliwa na changamoto ya mabadiliko ya joto kati ya mazingira baridi ya ndani ya vyumba au magari yenye kiyoyozi na joto kali la nje.

Kukaa katika chumba kimoja na marafiki wapya pia kunaweza kuongeza ugumu, kwani kila mtu ana mapendeleo tofauti ya hali ya joto.

Hata hivyo, wasiwasi mkuu wa mabadiliko haya ya joto ni kuongezeka kwa hatari ya kupata mafua ya kawaida, Taher Doroudi, naibu mkuu wa Kituo cha Matibabu cha Hajj na Hija, aliiambia IQNA.

Ingawa kiyoyozi katika hoteli huleta ahueni na utulivu lakini kutoka nja katika mazingira ya joto kali kunaweza kuchosha. Hali hiyo hiyo hujikariri wakati wa kuingia na kutoka kwa magari yenye viyoyozi, na kusababisha muundo wa mabadiliko ya hali ya joto ambayo yanaweza kuwaacha Mahujaji katika hatari ya magonjwa ya kupumua, kulingana na mtaalam huyo.

"Ili kupunguza hatari hii, tunawashauri mahujaji kutumia viyoyozi kwa uangalifu katika vyumba vyao ambapo inashauriwa kudumisha hali ya joto ya wastani kati ya nyuzi 25 hadi 26," alisema.

Mara nyingi baadhi ya watu huweka chumba katika hali ya baridi ya nyuzii joto 17 hadi 20, ambayo inaweza kusababisha maswala ya kiafya, aliongeza.

Kidokezo cha vitendo ni kuweka kiyoyozi kikiendelea kufanya kazi ukiwa nje, na kukizima unaporudi kwenye chumba chako, ili kuhakikisha mazingira yana hali ya hewa inayoweza kustahamilika, Doroudi alisema.

Zaidi ya hayo, pamoja na kutaniko la watu, ni jambo la manufaa kuruhusu mzunguko wa hewa katika vyumba vya hoteli kwa kuweka madirisha wazi kwa saa moja au mbili kila siku, aliongeza.

"Aidha kunywa maji ya kutosha ni muhimu, tunashauri kujizuia kunywa maji au vinywaji baridi sana," alionya.

Badala yake, Mahujaji wanaweza kuchagua maji ambayo ni baridi ya kutosha kuburudisha bila kuwa baridi sana, kwani hii husaidia kuzuia magonjwa yanayohusiana na joto bila kuongeza hatari ya kupata mafua, aliongeza. Hivyo ni wazi kuwa kuongeza kiwango cha baridi katika kiyoyozi na pia kunywa maji baridi sana wakati wa joto ni mambo ambayo yanaweza kupelekea kupata mafua.

Hija ni safari ya kwenda Makka ambayo kila Mwislamu mwenye uwezo wa kimwili na kifedha analazimika kuitekeleza angalau mara moja katika maisha yake.

3488633

Habari zinazohusiana
Kishikizo: hija
captcha