IQNA

Maonesho ya Kaaba yazinduliwa Makkah kwa Mahujaji

20:52 - May 26, 2025
Habari ID: 3480742
IQNA – Maonesho mapya huko Makkah yanaonesha historia ya Kaaba kwa Mahujaji wanaohudhuria msimu wa Hija mwaka huu wa 1446 Hijria.

Mamlaka Kuu ya Masuala ya Msikiti Mkuu na Msikiti wa Mtume imezindua maonesho ya “Nyumba ya Kwanza,” yakitoa mwonekano wa kina wa historia ya Kaaba.

Maonesho hayo yako katikaeneo la  ndani ya Msikiti Mkuu wa Makkah, mkabala wa Lango la 100 (Lango la Mfalme Abdullah). Maonesho hayo yanakaribisha wageni kila siku kutoka saa 6 asubuhi hadi saa 4 usiku wakati wote wa Hija, kama ilivyoripotiwa na Saudi Gazette siku ya Jumapili.

 Yakisanifiwa kwa kuzingatia teknolojia ya kisasa na uhalisia wa kihistoria, maonesho hayo yanawaruhusu Mahujaji na wageni kufuatilia historia ya Kaaba—kutoka zama za Nabii Ibrahim, Amani iwe juu Yake, hadi enzi za kisasa.

Maonesho hayo yanatoa mwonekano wa kina wa umuhimu wa kihistoria na kiroho wa eneo hilo takatifu. Maonesho yanatumia mbinu za kidijitali, michoro yenye mwendo na skrini zinazoguswa.  Pia wageni wanaweza kuona mchakato wa kutengeneza Kiswa, ambachoni kitambaa chenye mapambo kinachofunika Kaaba.

Wageni pia wanaweza kujifunza kuhusu vifaa na mbinu zilizotumiwa kuithibiti kwa muda. Mamlaka hiyo imeeleza kuwa mpango huu ni sehemu ya juhudi pana za kuboresha uzoefu wa kiroho na kielimu kwa Mahujaji. Msimu wa Hija wa 2025, unaolingana na 1446H katika kalenda ya Kiislamu, unatarajiwa kushuhudia mamilioni ya Waislamu kutoka kote duniani wakikusanyika Makkah kwa ibada ya Hija ya kila mwaka.

3493234

Kishikizo: hija historia
captcha