IQNA

Ustawi wa Hija

Pango la Hira kupata huduma za magari ya nyaya angani ifikapo 2025

14:24 - August 19, 2024
Habari ID: 3479299
IQNA - Saudi Arabia imezindua mipango ya kuunda mfumo wa magari yanayotumia nyaya angani (cable cars) ili kuboresha ufikiaji wa Pango la Hira katika Jabal Al Noor, Makka, na mradi huo unatarajiwa kukamilika ifikapo 2025.

Mpango huu unalenga kuboresha huduma ya Hija, kuwezesha ufikiaji rahisi katika eneo hili muhimu la kihistoria na kidini, ambapo Mtume Muhammad (SAW) alipokea ufunuo au Wahy wake wa kwanza.

Magari hayo ya nyaya yatapanda hadi kwenye Pango la Hira, lililo kwenye mwinuko wa takriban mita 634 na takriban kilomita 4 kutoka Msikiti Mkuu.

Mradi huu ni sehemu ya mpango mpana zaidi unaojumuisha kukamilika kwa Wilaya ya Utamaduni ya Hira na uzinduzi wa makumbusho matatu mapya huko Jabal Omar katika mwaka huo huo, kulingana na vyombo vya habari vya Saudi.

Jabal Al Noor, inayojulikana kwa sura yake ya kipekee kama nundu ya ngamia na miteremko mikali, ina umuhimu mkubwa kwa Waislamu kutokana na umuhimu wa kihistoria wa pango hilo.

Saudi Arabia to Introduce Cable Car System for Easier Access to Hira Cave by 2025

3489544

Kishikizo: hija treni
captcha