IQNA

Mayahudi katika Qur'ani / 4

Idadi kubwa ya Aya za Qur'ani kuhusu Mayahudi

17:59 - June 05, 2024
Habari ID: 3478938
IQNA - Kuna aya nyingi ndani ya Qur'ani Tukufu kuhusu Mayahudi walioishi wakati wa uhai wa Nabii Musa (AS) na wale walioishi katika miaka ya mwanzo baada ya kuja kwa Uislamu.

Hii ina hekima iliyofichika ambayo inaweza kuendelea hadi zama za kisasa.

Aya nyingi ndani ya Qur'ani Tukufu zinazungumzia kisa cha Bani Israil, walichokifanya wakati wa utume wa Musa (AS) na baadae, na tabia zao na mwenendo wao katika historia, hata wakati wa kuteremshwa Quran huko Madina.

Idadi hii kubwa ya aya inapaswa kuwafanya Waislamu kuwa makini na suala hili. Wanapaswa kuwaza na kutafakari ni kwa nini Mwenyezi Mungu amewataja Wayahudi na mwenendo wao zaidi ya mataifa mengine kuwa ni mfano na somo kwa watu wote.

Wayahudi walifanyaje kwamba kuna maonyo mengi juu yao? Na muhimu zaidi, ni nini imekuwa chimbuko na sababu ya msingi ya walichokifanya Bani Isra’il? Je, aya hizi za Qur'ani zinawahusu tu Wayahudi walioishi katika miaka ya mwanzo baada ya kuja kwa Uislamu au pia zinahusu mustakabali na zinaweza kutumika kwa Uzayuni wa zama hizi pia?

Jambo moja linaweza kuwa ukweli kwamba hatima ya Bani Isra'il ina mambo mengi yanayofanana na yale ya Waislamu. Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) amenukuliwa akisema: “Umma wangu utafuata nyayo za Bani Isra’il,  na kutenda kama wao kiasi kwamba wakiingia kwenye shimo, hawa pia watawafuata kwenye shimo hilo.

Nukta nyingine inaweza kupatikana kwa kuyapitia matukio yaliyotokea baina ya Mayahudi na Mtukufu Mtume (SAW).

Kuna misimamo miwili ndani ya Qur'ani kuhusiana na Mayahudi, inawazingatia baadhi yao kuwa ni watu wa imani na matendo mema na kundi la pili ni wale wanaovunja ahadi zao.

Kwa mujibu wa Qur'ani, kundi la pili lina uadui wa hali ya juu kabisa dhidi ya Waislamu: " . Hakika utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa walio amini ni Mayahudi na washirikina..." (Aya ya 82 ya Suratul-Maidah)

Uadui wa Mayahudi dhidi ya Waislamu haukupungua baada ya Mtukufu Mtume (saww) bali uliongezeka zaidi, huku kukiwa na njama nyingi na madhara yaliyowapata Waislamu kutoka kwa Wayahudi. Quran inasema: "Hayo uliyoteremshiwa wewe (Muhammad) kutokana na Mola wako Mlezi yatawazidishia wengi katika wao uasi na ukafiri. Basi usiwasikitikie watu makafiri. (Aya ya 68 ya Suratul-Maidah)

Katika ulimwengu wa kisasa pia, Wazayuni wameonyesha chuki kubwa dhidi ya Uislamu na Waislamu kwa njia mbalimbali, jambo ambalo linalazimu juhudi za Waislamu kuwajua na njia za kukabiliana na tishio lao. Na itakuwa bora kumjua adui huyu kwa mtazamo wa mafundisho ya Qur'ani Tukufu na Uislamu.

3488494

captcha