IQNA

Msikiti wa Paris Unachukizwa na Vyombo vya Habari na Mashambulio ya Kisiasa dhidi ya Uislamu

19:06 - June 24, 2024
Habari ID: 3479010
IQNA - Msikiti Mkuu wa Paris umelaani mwenendo unaoongezeka wa mashambulizi ya kisiasa na vyombo vya habari dhidi ya Uislamu nchini Ufaransa.

Msikiti huo ulisema katika taarifa yake kwamba mashambulizi hayo ya chuki dhidi ya Uislamu yameongezeka katika miezi ya hivi karibuni huku nchi hiyo ikipiga kura katika uchaguzi wa Umoja wa Ulaya EU) na inajiandaa kupiga kura katika uchaguzi mkuu hivi karibuni.

Uchaguzi wa mapema wa wabunge unatarajiwa kufanyika nchini Ufaransa katika awamu mbili mwezi, Juni 30 na Julai 7,2024, ili kuwachagua wajumbe 577 wa Bunge la 17 la Jamhuri ya Tano ya Ufaransa.

Msikiti Mkuu wa Paris umesema katika taarifa yake kwamba kuna matumizi mabaya ya kimfumo ya Uislamu na taswira mbaya ya dini hiyo katika mazungumzo ya kisiasa.

Imetoa wito wa kuongeza ufahamu kuhusu Uislamu na kuwataka wanasiasa kuacha kuushambulia Uislamu na Waislamu na badala yake wazingatie changamoto halisi katika jamii.

Taarifa hiyo pia ilisisitiza haja ya kuheshimiana na kujitolea kusikiliza sauti za watu.

Ikiwa na takriban watu milioni sita wa imani au asili ya Kiislamu, Ufaransa ni nyumbani kwa mojawapo ya jumuiya kubwa zaidi za Kiislamu barani Ulaya.

Wakati uchaguzi wa bunge wa haraka nchini humo unakaribia, wapiga kura Waislamu wanazidi kuwa na wasiwasi kuhusu matarajio ya ushindi wa mrengo mkali wa kulia, wakihofia vikwazo vinavyoweza kufuata.

Na vile vile Algeria, yatoa wasiwasi juu ya kuongezeka kwa chuki dhidi ya Uislamu nchini Ufaransa.

Hali kadhalika baadhi ya wale wanaofanya kampeni katika uchaguzi huo wameushambulia Uislamu na Waislamu, wakiapa kuweka vikwazo zaidi kwa alama na desturi za Kiislamu nchini iwapo watachaguliwa.

 

3488851

 

captcha