Maonyesho ya Qur’ani yatafanyika katika zaidi ya mikusanyiko mia moja ya waombolezaji wakati wa miezi ya Muharram na Safar, Hujat-Al-Islam Majid Babakhani, mkuu wa shirika linalosimamia mikusanyiko ya maombolezo, aliambia mkutano na waandishi wa habari Jumapili.
Maonyesho haya, yenye jina la "Qur’anI na Upinzani," yanawasilisha dhana za Qur'ani kupitia sanaa, picha, na mabango, aliongeza.
"Hatuwezi kuwataja Ahlul-Bayt (AS) bila pia kurejea kwenye Qur’anI, wala hatuwezi kujadili Qur’an na kuwapuuza Ahlul-Bayt (AS)," alisema.
Kitabu cha Marejeo ya Qur'ani kwa Imam Hussein (AS) Kimezinduliwa
Mipango imeandaliwa kwa ajili ya maandamano ya maombolezo ya Muharram kuzamishwa katika anga ya Qur'ani zaidi, alibainisha afisa huyo.
"Hii inajumuisha matumizi ya umaridadi ya mada na sanaa za Qur'ani, na kujihusisha na aya na dhana za Qur'ani ili kuwasaidia waombolezaji kuzifahamu vyema baadhi ya aya zilizochaguliwa," aliongeza.
Moja ya programu hizi inahusisha kupitia na kufasiri aya zilizosomwa na Imam Hussein (AS) katika safari ya kutoka Madina kwenda Makka na kutoka Makka hadi Karbala, kwa mujibu wa Babakhani.
"Somo muhimu zaidi tunaloweza kujifunza kutokana na mauaji ya Ashura ni ushindi wa haki dhidi ya uovu," alisisitiza.
Hamburg Yaandaa Semina ya Uzinduzi ya Ashura kwa Makhatwibu wa Ulaya,
Muharram ni mwezi wa kwanza katika kalenda ya mwandamo ya Hijri.
Waislamu wa madhehebu ya Shia na wengineo katika sehemu mbalimbali za dunia hufanya sherehe kila mwaka katika mwezi wa Muharram kuomboleza kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hussein (AS) na masahaba zake.
Imamu wa tatu wa Shia (AS) na kikundi kidogo cha wafuasi wake na wanafamilia wake waliuawa kishahidi na dhalimu wa zama zake - Yazid Bin Muawiya, katika vita vya Karbala katika siku ya kumi ya Muharram (ijulikanayo kama Ashura) mwaka wa 680. AD.