IQNA

Ahlul Bayt (AS)

Maonyesho ya picha za Maeneo Matakatifu wa Mashia kuandaliwa barani Ulaya

16:48 - December 22, 2024
Habari ID: 3479938
IQNA – Toleo la pili la maonyesho ya maeneo matakatifu ya Shia yatafanyika katika vituo vya Kiislamu na kitamaduni barani Ulaya.

Maonyesho hayo yenye jina la Hubb al-Hussein Yajmauna (Mapenzi kwa Imam Hussein (AS) yanatuleta pamoja), yatafanyika kuanzia siku ya Mab'ath (kuashiria kuteuliwa kwa Muhammad (SAW) kuwa Mtume) hadi siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa Imam Mahdi (Mwenyezi  Mungu aharakishe ujio wake wenye furaha-ATF-), yaani kuanzia Januari 28 hadi Februari 15, 2025.

Picha zinazoonyeshwa kwenye maonyesho hayo zina makaburi matakatifu huko Najaf, Karbala, Samarra na Kadhimiya pamoja na matembezi ya kila mwaka ya Arbaeen nchini Iraq.

Vituo vya Kiislamu na kitamaduni katika nchi za Ulaya vilivyo tayari kuandaa maonyesho hayo vinahimizwa kuwasiliana na +4917679289366 kupitia WhatsApp au Telegram ili kuwasilisha ombi lao.

Arbaeen ni tukio la kidini linaloadhimishwa na Waislamu wa Shia katika siku ya arobaini baada ya Siku ya Ashura, ambayo ni siku ya kukumbuka kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) na Imamu wa tatu wa Shia.

Ni miongoni mwa safari kubwa zaidi za kidini za kila mwaka duniani, huku mamilioni ya Waislamu wa madhehebu ya Shia na wengineo wakitembea kuelekea Karbala kutoka miji mbalimbali ya Iraq na maeneo mengine ya dunia.

.  

Photo Exhibitions Featuring Shia Holy Shrines Planned in Europe

4255225

 
Habari zinazohusiana
captcha