Msemaji wa polisi wa KZN Brigedia Jay Naicker aliripoti kwamba polisi wa Greenwood Park wanachunguza kisa cha kupatikana na vilipuzi kinyume cha sheria.
Tukio hilo lilitokea Julai 8, 2024, mwendo wa saa 1:30 asubuhi kwenye Barabara ya Kenneth Kaunda. Washukiwa hao, ambao bado hawajatambuliwa, walikatishwa na gari la ulinzi lililokuwa likishika doria na baadaye wakakimbia, na kuvitupa vifaa hivyo kwenye eneo la msikiti huo, The Witness liliripoti Jumanne.
Brigedia Naicker alisema, "Mara moja alishuku kuwa ni vilipuzi na akawasiliana na mamlaka muhimu ambazo nazo ziliwasiliana na polisi."
Mafundi wa bomu kutoka idara ya polisi walithibitisha kuwa vitu hivyo vilikuwa ni vilipuzi vya kujitengenezea nyumbani vilivyoundwa na vifaa vya kibiashara.
“Vifaa havikuwekwa ili kulipuka, Inashukiwa kuwa wanaume hao walikuwa wakielekea eneo lisilojulikana wakiwa na vifaa hivyo walipotatizwa na afisa wa usalama,” Naicker aliongeza kwa kusema ; Msako wa kuwatafuta washukiwa hao unaendelea kwa sasa.
Waislamu wa Afrika Kusini Wahimizwa Kushiriki Kisiasa Zaidi
Wadhamini wa Msikiti wa Durban Kaskazini, unaojulikana pia kama Musjidur Rahman, walitoa taarifa kuhusiana na tukio hilo.
"Msikiti umeimarisha hatua za usalama, na kumtaka mtu yeyote aliye na taarifa au nia ya jaribio la shambulio la bomu, au ambaye anaweza kuwa karibu na tukio hilo, kuwasiliana na vyombo vya sheria au msikiti moja kwa moja," ilisema taarifa hiyo.
“Kitendo hiki cha aibu hakitazuia jamii ya Kiislamu kutekeleza imani yao au kujihusisha na mazungumzo na imani nyingine.
Msikiti unabaki wazi, kuwakaribisha wageni kama kawaida,” ilisema taarifa hiyo.