Vikosi vya dharura vinavyowasaka Wapalestina walioaga dunia viliripoti kwamba miili mingi iliyopatikana ni ya wanawake na watoto.
Miili hiyo ilipatikana ikioza mitaani baada ya vikosi vya Israel kurudi nyuma siku ya Ijumaa asubuhi, na hivyo kuhitimisha operesheni ya siku saba katika eneo hilo.
Wafanyikazi wa ulinzi wa raia waliendelea kuokoa waliokufa kutoka kwa barabara na majengo yaliyoharibiwa.
"Takriban miili 60 ilihesabiwa, Baadhi ya miili ilizikwa papo hapo, Wengine walipelekwa katika hospitali za karibu. Miili mingi bado iko chini ya vifusi.
Vikosi vya utawala katili wa Israel viko karibu na juhudi za uokoaji hukatizwa mara kwa mara," Mahmoud Basal, mkurugenzi wa Ulinzi wa Raia wa Ukanda wa Gaza, aliiambia Al Jazeera.
"Kuna nyumba ambazo hatuwezi kufika, na kuna zile ambazo zilichomwa ndani ya nyumba zao," Basal aliongeza, akibainisha kuwa wengi wa waliouawa walikuwa wameondoka kwenye makazi ya karibu baada ya kuamriwa kuhama.
Vifo vya Ukanda wa Gaza vinaweza kuwa juu mara tano kuliko takwimu rasmi.
Basal pia alisema kwamba maiti katika Tal al-Hawa zilipatikana katika hali ya kuoza au kukatwakatwa sehemu na mbwa.
Na kulingana na vyanzo vya ndani vya Palestina, wengi wa wahasiriwa walikuwa wanawake na watoto.
Matokeo haya yanakuja huku Umoja wa Mataifa ukikadiria kuwa karibu Wapalestina 300,000 wamesalia kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.
Hali ya Tal al-Hawa ilifanana na ile ya wilaya ya Shujayea, kitongoji kingine katika Jiji la Gaza, ambapo vikosi vya utawala wa Israeli viliondoka siku ya Alhamisi kufuatia operesheni ya wiki mbili.
Mamlaka ziliripoti kupata miili 60 zaidi huko Shujayea, na mingi zaidi ikiwa imezikwa chini ya vifusi vya nyumba.
Wizara ya Afya ya Ukanda wa Gaza imeripoti kuwa zaidi ya watu 38,300 wameuawa hadi sasa kutokana na uvamizi wa utawala huo katili Israel, ulioanza Oktoba 2023, mwaka jana.