Huu ni msingi wa pili wa harakati ambayo Imam Hussein (AS) alianzisha dhidi ya Yazid kama ilivyotajwa katika barua ya Imam wa tatu (AS) kwa ndugu yake Muhammad ibn al-Hanafiyya.
Kwa mujibu wa baadhi ya Hadithi kuamrisha mema na kukataza maovu ni kama bahari ambayo mema mengine mbele yake ni tone la maji.
Qur’ani Tukufu katika aya nyingi inahusu kuamrisha mema na kukataza maovu kuwa ni wajibu wa waumini wote.
Kwa mfano, Mwenyezi Mungu anasema dhambi Aya ya 71 ya Sura At-Tawbah: “
Na Waumini wanaume na Waumini wanawake ni walinzi wao kwa wao; wanaamrisha mema, na wanakataza maovu, na wanashika Swala, na wanatoa Zaka, na wanamt'ii Mwenyezi Mungu na Mtume wake.
Hawa Mwenyezi Mungu atawarehemu; Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye hekima”
Kwa mujibu wa aya hii, kuwaamrisha waumini kuamrisha mema na kukataza maovu ni kwa sababu kuna urafiki na ushirikiano baina ya waumini katika jamii.
Waumini ni Walii (rafiki) wa kila mmoja wao na hii ina maana kwamba wanapaswa kusaidiana katika mambo mbalimbali.
Wanatakiwa kuhimizana kutenda mema na kuzuia maovu.
Kwa hiyo waumini wanahisi kuwajibika wao kwa wao na hawatachukizwa na yale ambayo ndugu yao katika imani anawaambia wafanye au wasifanye.
Misingi ya Qur’ani Tukufu ya Mauaji ya Imam Hussein (AS)
Hata hivyo, ikiwa mtawala wa jamii ni fisadi na dhalimu kama Yazid ibn Muawiyyah, angezuia kuanzishwa kwa jamii ya imani na matokeo yake ni kujengeka kwa urafiki na udugu baina ya waumini.
Angejaribu kuiweka jamii chini ya udhibiti wake kwa kuzusha migawanyiko na mifarakano baina ya makundi mbalimbali na kuwatesa waumini wa kweli kama Imam Hussein (AS).
Katika hatua hii, mtu kama Imam Hussein (AS) anaona kuwa ni wajibu wake kuinuka dhidi ya mtawala fisadi kama Yazid na kutengeneza njia ya utambuzi wa jamii ya imani, udugu, na urafiki kwa kumuondoa madarakani.
Kwa hivyo, namna kubwa kabisa ya kuamrisha mema na kukataza maovu ni kuinuka dhidi ya mtawala dhalimu.
3489103