IQNA

Haramu Tukufu ya Karbala na Taasisi ya Qur'ani ya Senegal kuimarisha ushirikiano

15:35 - May 12, 2025
Habari ID: 3480673
IQNA – Mshauri wa masuala ya Qur'ani katika Idara ya Mfawidhi wa Haram Tukufu ya Imam Hussein (A.S) amekutana na Rais wa Taasisi ya Kimataifa ya Qur'ani ya al-Muzdahar nchini Senegal kujadili njia za kuendeleza ushirikiano.

Sheikh Hassan al-Mansouri amesisitiza haja ya kupanua ushirikiano na taasisi hiyo wakati wa mkutano wake na Sharif Muhammad Ali Haidara.

Amesisitiza umuhimu wa kushirikiana katika njia ya kuitumikia Qur'ani Tukufu na kueneza mafundisho ya Qur'ani katika eneo la Afrika Magharibi, kama ilivyoripotiwa na tovuti ya imamhussein.org.

Pande zote mbili zilieleza uhusiano wa kina uliojengeka kwa zaidi ya miaka kumi na minne, na zilikubaliana kuendeleza ushirikiano huo, hasa kwa kuzingatia kupanuka kwa mwamko na mapokezi ya mafundisho ya Qur'ani katika nchi za Afrika Magharibi.

Mkutano huo ulikuwa sehemu ya mfululizo wa ziara na mashauriano ya mshauri wa masuala ya Qur'ani wa haramu na watu mashuhuri pamoja na taasisi za Qur'ani duniani.

Lengo kuu la mikutano hii ni kupanua wigo wa shughuli za Qur'ani na kubadilishana tajriba zilizofanikiwa katika ulingo huo mtukufu.

3493043

captcha