IQNA

Misikiti 100 itajengwa Sharjah, UAE

22:01 - September 12, 2024
Habari ID: 3479422
IQNA - Misikiti mia moja imepangwa kujengwa kuchukua nafasi ya misikiti mikongwe katika mji wa Sharjah, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Siku ya Jumatatu, mtawala wa Sharjah aliidhinisha mpango wa kujenga na kuchukua nafasi ya misikiti mikongwe iliyochaguliwa kote katika jiji hilo.

Chini ya mpango ulioidhinishwa Sultan bin Muhammad Al Qasimi, Mjumbe wa Baraza Kuu na Mtawala wa Sharjah, misikiti 100 itajengwa katika maeneo tofauti.

Mradi huo utagharibi Dirhamu milioni 800 ambapo kati misikiti 100, 40 ijajengwa mahalama pa misikiti ya kale na  60 itajengwa upya.

Sharjah ni mji wa tatu kwa watu wengi katika Umoja wa Falme za Kiarabu, baada ya Dubai na Abu Dhabi. Ni mji mkuu wa Imarati  ya Sharjah na ni sehemu ya eneo la mji mkuu wa Dubai-Sharjah-Ajman.

3489860

Kishikizo: sharjah misikiti
captcha