IQNA

Misikiti ya Misri yaandaa mihadhara kuhusu ‘Familia Katika Sira ya Mtume Muhammad (SAW)’

7:47 - August 02, 2025
Habari ID: 3481031
IQNA –Mihadhara kuhusu “Nafasi na Umuhimu wa Familia katika Sira ya Mtume Mtukufu Muhammad (SAW)” imefanyika katika misikiti mbalimbali nchini Misri.

Wizara ya Wakfu ya Misri iliandaa mihadhara 684 katika mikoa yote ya nchi, chini ya kaulimbiu isemayo:
“Bora wenu ni yule aliye mwema kwa familia yake, nami ni mbora kwa familia yangu”; Sira ya Mtume (SAW) ni mfano wa kuigwa katika kuiunga mkono familia.

Wizara hiyo imeweka katika ratiba yake ya kazi kutekeleza mipango ya elimu na maarifa katika misikiti, ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kueneza fikra ya wastani na mwanga wa elimu sahihi.

Mihadhara hiyo ilijikita katika kueleza nafasi ya familia katika Uislamu, uaminifu wa Mtume Muhammad (SAW) katika kuilea na kuiimarisha familia, pamoja na misingi aliyoianzisha katika mahusiano ya kifamilia kama vile huruma, uadilifu na ukweli.

Pia ilisisitizwa kuwa Sira ya Mtume (SAW) ni kielelezo bora cha maisha ya kifamilia yaliyojengwa juu ya mapenzi, heshima na kuelewana.

Kupitia mihadhara hii, Wizara ya Wakfu inalenga kuimarisha maadili halisi ya kifamilia katika jamii na kusisitiza kuwa utulivu wa familia ndio nguzo kuu ya kujenga jamii yenye afya njema. Maelekezo na nasaha za Mtume (SAW) ni rejea madhubuti katika malezi ya watoto na kukuza heshima baina ya wanandugu wa familia.

Kwa mujibu wa wizara, mihadhara hiyo, ambayo imepokelewa kwa hamasa kubwa kutoka kwa wananchi, imesaidia sana katika kuifanya misikiti kuwa vituo vya uelimishaji na uhamasishaji wa jamii, na sehemu ya kukuza maadili na tabia njema.

3494068

captcha