Wizara ya Mambo ya Kiislamu, Da’awah na Mwongozo pia imepiga marufuku kurushwa mubashara kwa Sala kwenye majukwaa yoyote ya vyombo vya habari bila idhini, kama ilivyoripotiwa na Shirika la Habari la Saudi (SPA).
Miongozo hiyo inasisitiza umuhimu wa maimamu na wahubiri kuzingatia sheria hizi na kwa waumini kudumisha nidhamu na adabu za kidini.
Hatua hizi, kulingana na wizara hiyo, zinalenga kulinda utakatifu wa misikiti na kuhakikisha mazingira ya ibada ya utulivu bila usumbufu wowote.
Sheikh Dk. Abdulrahman Al Sudais, Mkuu wa Masuala ya Kidini katika Msikiti Mkuu na Msikiti wa Mtume, alisisitiza dhamira ya wizara hiyo ya kuboresha huduma na mipango kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Aidha, wizara inapanga kuendesha mipango ya kidigitali ya Ramadhani, ikilenga kuboresha hali ya Mahujaji wa Umrah na wageni wa misikiti hiyo miwili mitukufu.
Mamlaka zinasema hatua hizi zinalenga kuunga mkono utekelezaji mzuri na wenye heshima wa ibada katika Mwezi mtukufu wa Ramadhani.
3491954