IQNA

Dokumentari yatayarishwa kutambulisha Misikiti muhimu ya Misri

18:24 - July 18, 2025
Habari ID: 3480960
IQNA – Wizara ya Wakfu (Awqaf) ya Misri imetangaza kutayarishwa kwa mfululizo wa dokumentari zitakazoangazia misikiti muhimu ya nchi hiyo.

Mpango huu dokumentari, unaojulikana kwa jina la "Misikiti Ina Historia", unalenga kutambulisha sifa za kihistoria, usanifu wa majengo (architecture), pamoja na mchango wa kimalezi na kidini wa misikiti muhimu nchini Misri. Pia utabainisha nafasi ya Wizara ya Awqaf katika kuhifadhi, kuendeleza na kukarabati misikiti hiyo, kwa mujibu wa ripoti ya El-Balad News.

Dokumentari  hizi zitapeperushwa kupitia mtandao wa satelaiti wa Misri, Al-Hayat, na zitalenga misikiti yenye hadhi ya kidini na kitaifa, kama vile:

  • Msikiti wa Sayyida Zainab (SA) Msikiti wa Imam Hussein (AS) Msikiti wa Sayyida Nafisa Msikiti wa Sayyida Fatima (SA)

Makala zitafafanua kuhusu mtindo wa kijengo wa kila msikiti, jukumu lake la kimalezi na kidini (da’wah), pamoja na historia yake tukufu.

Vipindi hivyo vitajumuisha picha halisi za misikiti ya kale na mahojiano na wanahistoria na maimamu wa misikiti mikuu. Hii itatoa maelezo ya kina na ya kielimu kuhusu historia ya misikiti hiyo pamoja na matukio muhimu na watu mashuhuri waliopita ndani ya misikiti hiyo kwa nyakati tofauti.

Lengo kuu la makala hizi ni kuinua uelewa wa hadhi na thamani ya misikiti mikubwa ya Misri, si kwa Wamisri tu, bali pia kwa Ummah wa Kiislamu kwa ujumla.

Mpango huu unatarajiwa kutoa maarifa ya kuaminika kwa makundi mbalimbali ya hadhira, ikiwemo vijana, watafiti, waumini, na walimu wa dini.

 

4294658

Kishikizo: misri misikiti
captcha