Ahmed Al Zahid, msemaji wa Tuzo ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Dubai (DIHQA) ametangaza kuwa, toleo la nane la Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Sheikha Fatima Bint Mubarak lilikamilika siku ya Ijumaa.
Sherehe ya kufunga ilifanyika katika Ukumbi wa Kongamano la Utamaduni na Sayansi huko Dubai, kufuatia ushiriki mkubwa kutoka nchi 62 na jumuiya za Kiislamu duniani kote.
Ameeleza kuwa mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu yalifanyika kuanzia tarehe 7 hadi 11 Septemba na siku ya Ijumaa, zawadi maalumu zilitolewa kwa washindi kumi bora. Aidha amesema washiriki wote pia walipata zawadi.
Al Zahid alisema toleo hili lilishuhudia uzinduzi wa tovuti mpya ya DIHQA. Tovuti hii itafikiwa na kila mtu na itawaruhusu watumiaji kuteua wagombeaji wa mashindano, kujifunza kuhusu matawi kumi na manne ya tuzo hiyo, na kutazama picha za historia ya tuzo tangu kuanzishwa kwake.
Mwishoni mwa mashindano ya mwaka huu, mshiriki wa Uswidi Safia Taher alipata nafasi ya kwanza, huku Khadija Al-Mukhtar kutoka Mauritania akishika nafasi ya pili. Fati Rashid kutoka Kenya alipata nafasi ya tatu. Maryam Habib kutoka Nigeria na Afnan Rashad kutoka Yemen walishikilia nafasi ya nne kwa pamoja. Asmaa Younis kutoka Misri alishika nafasi ya sita, na Asmaa Shalabi kutoka Tunisia alikuwa wa saba. Zahra Ansari kutoka Iran alishika nafasi ya nane, Putri Hanif kutoka Malaysia alikuwa wa tisa, naye Mona Al-Sagheer kutoka Libya alishika nafasi ya kumi na Aisha Jakhoura kutoka Afrika Kusini.
Tuzo la Kimataifa la Qur'ani Tukufu la Dubai (DIHQA) kila mwaka huandaa mashindano hayo ya kimataifa ya Qur'ani kwa wanawake kutoka nchi mbalimbali.
3489884