IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Iran kutuma mwakilishi Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani kwa wanawake Dubai­­­

23:22 - July 26, 2024
Habari ID: 3479186
IQNA - Zahra Ansari ambaye amehifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu ataiwakilisha Iran katika toleo la 8 la Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Sheikha Fatima Bint Mubarak Kwa Wanawake ya Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu.

Mashindano hayo hufanyika kila mwaka jijini Dubai kwa kushirikisha wanawake kutoka nchi mbalimbali.

Tuzo la Kimataifa la Qur'ani Tukufu la Dubai (DIHQA) huandaa tukio hilo la kimataifa la Qur'ani.

Toleo hili la shindano hilo huenda likafanyika mwezi Septemba.

Maafisa hao wa DIHQA walituma mwaliko kwa Shirika la Masuala la Wakfu na Hisani la Iran, wakiiomba kutuma mwakilishi kwenye shindano hilo.

Ansari alimaliza wa pili katika toleo la hivi punde zaidi la Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani ya Iran.

Pia ameshinda taji la kwanza katika toleo la 37 la mashindano ya Qur'ani ya nchi hiyo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu.

3489245

Habari zinazohusiana
captcha