IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Wahifadhi kutoka Nchi 70 wanahudhuria Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Dubai

15:47 - March 15, 2024
Habari ID: 3478517
IQNA - Duru ya mwisho ya toleo la 27 la Tuzo la Kimataifa la Qur'ani Tukufu la Dubai (DIHQA) inaendelea katika mji huo wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa kushirikisha wawakilishi kutoka nchi 70.

Fainali hizo zilianza baada ya swala ya Taraweeh iliyoswaliwa Jumanne usiku huku wahifadhi kutoka Cameroon, Malaysia, Jordan, Italia, Mauritius na Ufilipino wakionyesha vipaji vyao vya Qur'ani.

Wakati huo huo, Mamlaka ya Umeme na Maji ya Dubai (DEWA) imetangaza ufadhili wake kwa hafla hiyo ya kimataifa.

Ibrahim Mohammed Bu Melha, mshauri wa mtawala wa Dubai kwa masuala ya kitamaduni na kibinadamu na mkuu wa kamati ya maandalizi ya Tuzo hiyo, amepongeza hatua hiyo, akisema, "Tunazingatia ushirikiano na DEWA kama ushirikiano wa kimkakati.”

Mashindano hayo yatataendelea hadi Machi 22 wakati washindi watatangazwa na kutunukiwa katika hafla ya kufunga.

Mwakilishi wa Iran katika mashindano ya mwaka huu ni Amir Hadi Bayrami, mhifadhi wa Qur'ani nzima ambaye ni mlemavu wa macho.

Alifuzu kwa fainali hizo baada ya kujibu vyema maswali ya jopo la majaji katika awamu ya awali Jumamosi.

Mashindano hayo ya Qur’ani ambayo ni maarufu kama Tuzo la Kimataifa la Qur'ani Tukufu la Dubai (DIHQA) huandaliwa kila mwaka katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

3487565

Habari zinazohusiana
captcha