Jumla ya wanawake 90 kutoka nchi 19 wenye mafanikio katika nyanja mbalimbali za Qur’ani walienziwa katika hafla hiyo, ambayo ilihudhuriwa na Waziri wa Utamaduni wa Iran Seyed Abbas Salehi, Mfawidhi wa Haram Takatifu ya Imam Ridha (AS) Hujjatul Islam Ahmad Marvi, na maafisa wengine kadhaa.
Wazungumzaji kwenye kongamano hilo walisisitiza hali ya wanawake katika familia na jamii na kusema kwamba tangu ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ya mwaka 1979, wanawake Waislamu nchini wamenawiri na kutia fora katika nyanja mbalimbali za Qur’ani.
Walibainisha uwezo mkubwa wa wanawake wasomi na wanaharakati wa Qur’ani katika kuhudumu katika nyadhifa za uongozi. Pia walisisitiza haja ya wanawake kujumuisha mafundisho ya Qur’ani katika maisha yao binafsi na ya kijamii. Katika hotuba yake, Hujjatul Islam Ahmad Marvi alirejelea matamshi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyed Ali Khamenei kuhusu majaribio ya adui ya kuchochea mifarakano na kuunda mgawanyiko, akibainisha kwamba, kulingana na Kiongozi huyo, njia pekee ya kukabiliana na vitisho hivi ni kufuata mafundisho ya Qur’ani Tukufu.