Rabi’ah Faraq aligundulika kuwa na saratani alipoingia muongo wa 70 wa umri wake lakini Pamoja na hayo aliweza kuhifadhi Qur’an Tukufu alipokuwa akitibiwa katika hospitali ya Uhispania.
Aliweza kuhifadhi Juzuu 15 akiwa hospitalini na pia wakati huo, licha ya umri wake, aliweza kumaliza masomo yake ya chuo kikuu na kupata shahada ya BA.
Alikuwa akitaka kuhifadhi Quran tangu utotoni, na akiwa na umri wa miaka 75, ndoto yake hatimaye ilitimia.
Qur’ani Tukufu ndio Maandiko pekee ya kidini ambayo wafuasi wake wanaweza kuhifadhi.
Watu wasiohesabika katika kila umma wa Kiislamu wamehifadhi Qur’ani Tukufu tangu siku ya kwanza ilipoteremshwa.
Qur’ani Tukufu ina Juzuu (sehemu) 30, Sura 114 na aya 6,236.
4237393