IQNA

Muqawama

Hizbullah yalenga makao makuu ya Mossad jijini Tel Aviv kwa kombora la balestiki

12:07 - September 26, 2024
Habari ID: 3479492
IQNA-Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imetumia kombora la balestiki kulenga makao makuu ya shirika la kijasusi la Israel, Mossad huko Tel Aviv ikiwa ni kwa mara ya kwanza, suala lililosababisha wahka mkubwa na ving'ora katika mji huo na maeneo mengine ya Israel ikiwa ni pamoja na Netanya.

Mfumo wa kuzuia makombora ya balestiki wa Israel wa Arrow ulitumiwa  mjini Tel Aviv mapema jana atano, na kuwafanya wakazi wa mji huo kukimbilia mafichoni.

"Katika kuunga mkono watu wetu wa Palestina huko Ukanda wa Gaza, na katika kuunga mkono Muqawama wao wa kishujaa na wa heshima, na katika kulinda Lebanon na watu wake, Muqawama wa Kiislamu (Hizbullah) umerusha kombora la balestiki la 'Qader 1' leo Jumatano, saa 6:30 asubuhi na kulenga makao makuu ya Mossad katika viunga vya Tel Aviv," imesema taarifa ya Hizbullah.

"Makao makuu haya yanahusika na mauaji ya viongozi na ulipuaji wa vifaa vya mawasiliano (pager na walkie-talkies) nchini Lebanon", imeongeza taarifa hiyo. 

Hapo awali, Hizbullah ililenga kambi ya kijeshi ya Ilaniya ya Israel katika upande wa kaskazini wa maeneo yanayokaliwa kwa mabavu kwa kutumia makombora ya Fadi-1.

Kambi hiyo ina uhusiano na Idara ya 146 ya Wanajeshi wa Israel, ambayo ni sehemu ya Kamandi ya Kaskazini.

Kabla yya hapo pia, harakati ya Hizbullah ya Lebanon ilitangaza kuwa imeshambulia kwa makombora kadhaa ya Fadi-1, Fadi-2 na maroketi ya Katyusha viwanda vya kijeshi vya Kampuni ya Rafael, ambayo inajishughulisha na vifaa vya kielektroniki, kaskazini mwa mji wa Haifa huko Israel.

Hizbullah pia ilishambulia mara mbili kambi ya kijeshi na uwanja wa ndege wa Ramat David kwa makumi ya makombora ya Fadi-1 na Fadi-2 kujibu mashambulio ya Israel yaliyolenga maeneo mbalimbali ya Lebanon na kusababisha vifo vya raia.

3490037

Habari zinazohusiana
Kishikizo: hizbullah lebanon mossad
captcha