IQNA

Harakati ya Hizbullah iko mstari wa mbele katika vita dhidi ya corona

18:50 - March 28, 2020
Habari ID: 3472610
TEHRAN (IQNA) – Harakati ya Hizbullah ya Lebanon iko mstari wa mbele kukabiliana na ugonjwa hatari wa COVID-19 au corona katika nchi hiyo ya Kiarabu.

Kwa mujibu wa tovuti ya Televisheni ya Al Manar, maafisa wa Hizbullah wanatekeleza oparesheni za kunyinyiza kemikali za kuua virusi vya corona katika miji na vijiji na pia kusambaza chakula na vifaa vya kiafya kwa wananchi ambao wametakiwa wabakie majumbani mwao ili kuzuia kuenea ugonjwa huo.

Wasimamizi wa miji na vijiji wamepongeza jitihada hizo za Hizbullah na pia harakati jumla za Hizbullah za kulinda taifa la Lebanon mbele ya uhasama wa utawala wa Kizayuni na pia katika masuala ya kitiba na kijamii.

Mapema wiki hii, Hizbullah ilisema wanachama wake wapatao 25,000, wakiwemo madaktari na wafanyakazi wa sekta ya afya, watahusika katika oparesheni za kukabiliana na corona.  Aidha Harakati ya Hizbullah imesema inachangia vifaa vya kitiba katika hospitali za Lebanon ambazo ziko mstari wa mbele kuwatibu wagonjwa wa COVID-19.

Mkuu wa Baraza la Utendaji la Hizbullah, Sayyed Hashim Safiyuddin amesema jukumu lao ni kuisaidia serikali na si kuchukua mahala pa serikali. Ameongeza kuwa, kwa ujumla Hizbullah itatuma madaktari 1,500, wauguzi 3,000 na wanaharakati 20,000 katika oparesheni ya kukabiliana na corona.

Hadi sasa Lebanon imerekodi kesi 412 za corona na tayari watu 8 wameshapoteza maisha kutokana na ugonjwa huo ambao umeenea kote duniani.

3887820

captcha