IQNA

8:42 - August 17, 2019
News ID: 3472087
TEHRAN (IQNA) -Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon ametahadharisha kuwa vita dhidi ya Iran ni sawa na vita dhidi ya mhimili mzima wa muqawama (mapambano ya Kiislamu) na kwa msingi huo amesisitiza kuwa: "Vita dhidi ya Iran vitawasha moto katika eneo lote ( Asia Magharibi)."

Sayyid Hassan Nasrallah Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon ameyasema hayo Ijumaa wakati akihutubu kwa njia ya Televisheni mjini Beirut kwa mnasaba wa vita vya sikuu 33 na huku akitoa pongezi kufuatia ushindi huo amesema: "Hatua ya Iran kutungua ndege ya kijasusi isiyo na rubani ya Marekani na pia kusimamisha meli ya mafuta ya Uingereza kwa mara nyingine ni thibitisho kuwa ina ushujaa."

Sayyid Nasrallah amesema kushindwa Marekani kutangaza vita dhidi ya Iran kufutia kutunguliwa drone hiyo ni ushindwa mkubwa. Ameongeza kuwa: "Rais Donald Trump wa Marekani ameweza kudiriki nguvu za kijeshi za Iran."

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameendelea kusema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel, Saudi Arabia, Imarati na baadhi ya tawala za Kiarabu katika Ghuba ya Uajemi zinataka eneo litumbukie katika vita na kuongeza kuwa: "Hizbullah inataka vita  visitishwe Yemen na Syria sambamba na kuwepo uthabiti Lebanon na Iraq."

Sayyid Nasrallah amebainisha kuwa, Harakati ya Hizbullah ya Lebanon sasa imegeuka na kuwa kundi lenye nguvu kubwa katika eneo la Asia Magharibi na huku akiwahutubu wakuu wa utawala wa Israel amesema: "Iwapo mtaivamia Lebanon, basi tutarusha hewani moja kwa moja maangamizi ya wanajeshi wa Israel."

Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon ameashiria pia mashambulizi ya muungano wa kijeshi wa Saudia dhidi ya Yemen na kusema: "Kutegemea mhimili wa muqawama kumepelekea wavamizi wasimamishwe na hivi sasa kuna bishara za kukaribia kusambaratika wavamizi."

Sayyid Nasrallah amesema leo Lebanon inashuhudia usalama na amani na kuongeza kuwa: "Hizbullah ya Lebanon iko katika hali ya utayarifu mkubwa kwa ajili ya kukabiliana na adui."

3835282/

Name:
Email:
* Comment: