IQNA

Sayyed Hassan Nasrallah kwa masaba wa Nisf Shaaban

Utawala wa Kizayuni una hofu kuwa uhai wake hautapita miaka 80

11:36 - April 08, 2020
Habari ID: 3472644
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema, hivi sasa katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel) kuna utawala ghasibu ambao una hofu una hofu kuwa uhai wake hautazidi miaka 80.

Sayyid Hassan Nasrallah ameyasema hayo usiku wa kuamkia leo, katika hotuba ya moja kwa moja kupitia Televisheni ya Al Manar kwa mnasaba wa mkesha wa Shaaban 15 (Nisf Shaaban), siku ya kuadhimisha mazazi yenye baraka ya Imam Mahdi (Ajjala-Allahu Ta'ala Farajahu Sharif- Mwenyezi Mungu Aharakishe Kudhihiri Kwake), Imam wa 12 wa Waislamu wa madhehebu ya Shia.

Kiongozi wa Hizbullah amesema Wazayuni wana hofu na wasiwasi juu ya kudhihiri Imam Mahdi (Mwenyezi Mungu Aharakishe Kudhihiri Kwake).

Sayyid Hassan Nasrallah ametoa mkono wa heri na pongezi kwa mnasaba wa siku hiyo yenye baraka na kueleza kwamba, kuzaliwa kwa Imam Mahdi (ATF) ni sawa na kuanza kukaribia zama za kuthibiti ahadi ya Mwenyezi Mungu; na akaongezea kwa kusema: Atakapodhihiri Imam Mahdi - Mwenyezi Mungu Aharakishe Kudhihiri Kwake-ataujaza ulimwengu uadilifu, amani na upendo.

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ametoa mkono wa pole pia kwa mnasaba wa kumbukumbu ya siku aliyouawa shahidi Ayatullah Muhammad Baqir Sadr pamoja na ndugu yake wa kike Bintul-Huda kwa amri  ya dikteta wa Iraq Saddam; na akamuenzi na kumtaja Ayatullah Sadr kuwa ni mwanafalsafa na mwanafikra mkubwa.

Sayyid Hassan Nasrallah alinukuu maneno aliyosema shahidi Sadr kuhusu Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na mwasisi mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Imam Khomeini (MA) na akasema: Wakati Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yalipopata ushindi, shahidi Sadr alisema: Imam Khomeini (as) amewezesha kuthibiti lile walilokuwa wakilitaka Manabii.

Katibu Mkuu wa Hizbullah amenukuu maneno mengine pia aliyotamka shahidi Ayatullah Muhammad Baqir Sadr alipousia kwa kusema: "Yeyukieni kwa Imam Khomeini kama yeye Imam alivyoyeyukia kwenye Uislamu" na akasisitiza kuwa, ufuataji wa wasia huo na njia hiyo utaendelea.

Mwanzoni mwa hotuba yake, Sayyed Nasrallah ametoa shukrani zake za dhati kwa wafanyakazi wote wa sekta ya afya kutokana na jitihada zao za kupambana na ugonjwa wa COVID-19 au corona.

3890010

captcha