IQNA

Nasrallah: Israel ni utawala wa muda unaokaribia kusambaratika

23:30 - February 16, 2022
Habari ID: 3474934
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Harakati ya Hizbuallah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrallah amezilaani nchi za Waislamu ambazo zimeanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel na kuutaja utawala huo kuwa ni ‘utawala wa muda’ ambao unaelekea kusambaratika.

Akizungumza kwa njia ya televisheni Jumatano, aidha amesema Israel ni utawala pekee duniani ambao sasa unajulikana kama utawala wa apathaidi huku akisema maafisa wa utawala huo wamekiri kuwa wanakabiliwa na changamoto ya kuhakikisha utawala huo unaendelea kuwepo.

Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon pia amesema harakati hiyo sasa inajiundia ndege zisizo na rubani au drone na makombora yenye uwezo wa kulenga shabaha kwa ustadi mkubwa.

Nasrallah amesema Hizbollah imweza kupata mafanikio hayo kwa kujitegemea na kuongeza kuwa, “tumekuwa tukiunda drone kwa muda mrefu nchini Lebanon na yeyote anayetaka tunakuweza kumuuzia.”

Aidha amesema Hizbullah ina uwezo wa kuimarisha uwezo wa maroketi yake kukabiliana na tishio la Israel. Kiongozi wa Hizbullah ameyasema hayo kwa mnasaba wa kukumbuka kuuawa shahidi viongozi wa harakati ya muqawama au mapambano ya Kiislamu  Sheikh Ragheb Harb, Sayyed Abbas al-Mousawi and Imad Mughniyeh.

Sayyed Nasrallah amesema tokea mwaka 1982 Harakati ya Hizbullah imekuwa ikilinda Lebanon kwa kukabiliana na vitisho vya Israel.

 

4036900

captcha