IQNA

Harakati ya Hizbullah
14:56 - May 26, 2022
Habari ID: 3475296
TEHRAN (IQNA)- Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa misaada yake na kwamba, haikusita hata kidogo kuisaidia Lebanon.

Akihutubu kwa mnasaba wa kukombolewa ardhi ya Lebanon kutoka katika makucha ya utawala dhalimu wa Israel na Siku ya Muqawama, Sayyid Hassan Nasrallah ameongeza kuwa, misaada ya Iran kwa Lebanon na Hizbullah ni jambo lisilo na kificho hususan mchango mkubwa wa shahidi Qassem Soleimani.

Kadhalika amesema: Tunalishukuru pia jeshi la Lebabon kutokana na hatua zake katika miaka ya hivi karibuni hasa kutokana na mshikamano wake na muqawama kama ambavyo tunalishukuru jeshi la Syria na makundi ya muqawama huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Kwingineko katika hotuba yake, Katibu Mkuu wa Hizbullah sambamba na kuuonya utawala haramu wa Israel amesisitiza kuwa, hatua yoyote iliyo dhidi ya Msikiti wa al-Aqsa italilipua eneo la Asia Magharibi.

Sayyid Hassan Nasrallah ameitaja tarehe 25 Mei kuwa moja ya masiku ya Mwenyezi Mungu na kwamba, ni miongoni mwa masiku ya kutimia ahadi ya Mwenyezi Mungu kwa Mujahidina.

Katibu Mkuu wa Hizbullah amewataka Walebanon kutambua sura halisi ya utawala ghasibu wa Israel.

Kuhusiana na matukio ya Palestina, Nasrullah amesema, hatua ya Israel ya kung'ang'ania kuuhujumu Msikitii wa al-Aqswa na kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu katika mji wa Quds zitapelekea kuibuka mlipuko mkubwa katika eneo la Asia Magharibi na kufuatiwa na matokeo yasiyofurahisha.

3479056

 

Kishikizo: nasrallah ، hizbullah ، palestina ، lebanon ، hizbullah
Jina:
Baruapepe:
* maoni:
* captcha: