IQNA

Qiraa

Qari wa Misri akisoma aya za Surah Hud katika Mashindano ya Qur’ani Uingereza (+Video)

20:35 - November 08, 2024
Habari ID: 3479717
IQNA - Qari wa Misri Ahmed al-Sayyid al-Qaytani alishika nafasi ya kwanza katika kategoria ya qiraa au usomaji Katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani nchini Uingereza wiki iliyopita.

Mashindano hayo ambayo pia yanajulikana kamaHabib ul-Quran yaliandaliwa katika mji wa Batley huko West Yorkshire, Uingereza, kuanzia Oktoba 31 hadi Novemba 3.
Al-Qaytani, 23, aliwashinda maqari kutoka nchi tofauti kama Morocco, Indonesia, Uingereza, Uhispania, Algeria, Bangladesh na Pakistan na kushinda tuzo ya juu katika kitengo cha qiraa.
Hapo awali alishinda tuzo katika matukio mengine ya kimataifa ya Qur'ani yakiwemo yale ya Iran, Misri na Qatar.
Katika tukio la Qur'ani la Uingereza, alisoma Aya ya 16 hadi 18 ya Surah Hud:


Hao ndio ambao hawatakuwa na kitu Akhera ila Moto, na yataharibika waliyo yafanya, na yatapotea bure waliyo kuwa wakiyatenda.
Basi je, mtu aliye na dalili wazi itokayo kwa Mola wake Mlezi, inayo fuatwa na shahidi anaye toka kwake, na kabla yake kilikuwa Kitabu cha Musa kilicho kuwa mwongozi na rehema - hao wanamuamini, na anaye mkataa katika makundi, basi Moto ndio pahala pa miadi yao. Basi usiwe na shaka juu ya hayo. Hii ni Haki itokayo kwa Mola wako Mlezi; lakini watu wengi hawaamini.
Na nani aliye dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye mzulia Mwenyezi Mungu uwongo? Hao watahudhurishwa mbele ya Mola wao Mlezi, na mashahidi watasema: Hawa ndio walio mtungia uwongo Mola wao Mlezi. Laana ya Mwenyezi Mungu iwapate walio dhulumu.

3490594

captcha