Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uingereza, video iliyosambazwa kwenye jukwaa la mitandao ya kijamii X inaonyesha mtu asiyejulikana akijaribu kuchoma moto nakala ya Qur'ani Tukufu.
Wakati huo, mpita njia alimpkonya mhalifu hiyo Qur'ani Tukufu iliyokuwa ikiteketea mikononi mwake na kumwangusha chini.
Kwa mujibu wa polisi wa eneo hilo, walipokea taarifa ya tukio hilo saa nane mchana.
Mtu huyo aliyevunjia heshima nakala ya Qur'ani Tukufu alijeruhiwa wakati wa tukio hilo. Polisi walieleza kuwa maafisa walifika eneo la tukio ndani ya dakika chache na kumkamata mtu aliyezuia jaribio la kuvunjia heshima Qur'ani Tukufu, kwa madai ya kumjeruhi mtu mwingine. "Mtu huyo yupo kizuizini na uchunguzi unaendelea," msemaji wa Polisi wa Metropolitan alisema.
3491862