IQNA

Mchoma Qur'ani jijini London aachiliwa kwa dhamana

21:11 - February 16, 2025
Habari ID: 3480226
IQNA – Mwanaume aliyachoma nakala ya Qur'ani Tukufu nje ya ubalozi mdogo wa Uturuki katikati ya London siku ya Alhamisi ameachiliwa huru kwa dhamana.

Hamit Coskun, 50, kutoka Derby, amekanusha mashtaka ya kuhusika na uchochezi wa kidinii. 

Katika video ya tukio, Coskun anasikika akiwatuhumu Waislamu kuwa ni ‘magaidi’ na hapo mwanamume mwingine akiwa na kisu alimpiga mateke na kumtemea mate. 

Mtu mwingine aliyekuwa kwenye baisikeli pia alionekana akimpiga mateke mhalifu hiyo aliyevunjia heshim Qur’ani Tukufu. 

Katika Mahakama ya Westminster Magistrates' Court Jumatatu, Coskun alizungumza kupitia mkalimani wakati alipokana kuhusija na uhalifu huo.. 

Alichukwa malipo ya kifungo na atashuhudia mbele ya mahakama hiyo kwa kusudi kwa tarehe 28 Mei. 

Mwanamume mwingine, Moussa Kadri, 59, kutoka Kensington na Chelsea, amefunguliwa mashtaka ya kumshambulia mhalifu huyo na atafikishwa kizimbani Jumanne.

3491873

captcha