IQNA

Ulindi

Amiri Jeshi Mkuu wa Iran asisitiza kuhusu kuongeza utayari na uwezo wa kivita wa vikosi vya ulinzi

19:57 - November 27, 2024
Habari ID: 3479819
IQNA-Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Iran amesema, kuongeza utayari na uwezo wa kivita ndilo jukumu muhimu zaidi la vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, ambaye pia niAmiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Iran, ameyasema hayo leo Jumatano alipokutana na maafisa na makamanda wa Jeshi la Wanamaji la Iran, ambapo sambamba na kuienzi kumbukumbu ya Novemba 28, 1980 ya maadhimisho ya hamasa iliyoonyeshwa siku hiyo na manowari ya Peikan katika kukabiliana na adui wa Kibaathi, na kupelekea kuitwa Siku ya Jeshi la Wanamaji, amesisitiza kuwa jeshi la Wanamaji lina umuhimu mkubwa na mchango wa kipekee katika dunia ya leo.

Amepongeza kazi zinazofanywa na vitengo mbalimbali vya operesheni, intelijensia, utoaji msukumo, ujenzi na ubunifu katika Jeshi la Wanamaji la Iran na akasema: mwelekeo wa vikosi vya ulinzi vya Iran hususan Jeshi la Wanamaji katika kazi na mipango yote inapasa ujikite katika kuongeza utayari na uwezo wa kivita.

Ayatullah Khamenei amesema, kuongezwa uwezo wa kivita kutawezesha kuzuia hujuma za adui na akaongeza kuwa: "kazi muhimu zaidi ya vikosi vya ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ni kuzuia uvamizi, kwa hivyo inapasa muufanye utendaji na uwezo wa kivita wa nchi uonekane mkubwa mbele ya macho ya wanaoitakia mabaya Iran ili wahisi kwa maana halisi kwamba makabiliano yoyote yatakayotokea yatawasababishia hasara kubwa".

Mwanzoni mwa mkutano huo, Admeri Shahram Irani, Kamanda Mkuu wa Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, alitoa ripoti kuhusu mipango na shughuli za kikosi hicho katika vitengo mbalimbali.../

 

4250855

Habari zinazohusiana
captcha