Ayatullah Sayyid Ali Khamenei ametoa ujumbe huo wa maneno kwa Muqawama wa Lebanon na kusisitiza kwa kusema: "Hatuna tofauti na nyinyi. Tuko pamoja nanyi. Sisi na nyinyi ni kitu kimoja. Machungu yenu ni machungu yetu, mateso yenu ni mateso yetu. Hakuna tofauti baina yenu na sisi, sote ni kitu kimoja."
Ujumbe huo wa Kiongozi Muadhamu umewasilishwa na msoma mashairi ya kidini wa Iran, Meysam Motiee, ambaye ameelekea Lebanon kama sehemu ya kampeni ya kitaifa ya Iran ya kuwafikishia misaada watu wanaodhulumiwa wa Ukanda wa Ghaza na Lebanon.
Motiee ameelekea Lebanon akiandamana na kundi la wanaharakati waliowatembelea wananchi mashujaa wa Lebanon kwa ajili ya kufikisha msaada wa kibinadamu wa Iran.
Shirika la Hilali Nyekundu la Iran limetangaza kuwa limeshapeleka tani 2,200 za msaada kwa wananchi wanamuqawama wa Lebanon. Imekuwa vigumu kwa Iran kuwafikishia misaada ya kutosha Wapalestina kutokana na vizuizi vinavyowekwa na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Tangu mwezi Oktoba 2023, Israel imekuwa ikifanya jinai za kutisha na ukatili wa pande zote dhidi ya wananchi wa Ukanda wa Ghaza na Lebanon ambapo imewafungia njia zote wananchi wa Ghaza na hairuhusu msaada wowote wa maana kuwafikia Wapalestina. Mashambulizi ya kikatili ya utawala haramu wa Israel yamepelekea zaidi ya Wapalestina 44,000 kupoteza maisha tokea Oktoba mwaka jana, wengi wao wakiwa wanawake na watoto huku karibu wakazi wote milioni mbili na nusu wa eneo hilo wakilazimika kuondoka katika makazi yao. Aidha srael imeua takribani Walebanoni 3,510 na kuwafanya malaki ya wengine kuwa wakimbizi.
4249104