Wakati wa ziara hiyo jioni ya Jumatatu, Kiongozi Muadhamu alipata taarifa kuhusu maendeleo ya matibabu ya kiongozi huyo mwandamizi wa kidini.
Awali, viongozi wengine kadhaa wa Iran, wakiwemo Rais Masoud Pezeshkian na Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu Meja Jenerali Hossein Salami, walikuwa wamemtembelea mwanazuoni huyo hospitalini.
Walimuomba Mwenyezi Mungu amponye Ayatullah Nouri Hamedani. Ayatullah Nouri Hamedani ni moja kati ya Marjaa Taqlid wa Waislamu wa madhehebu ya Shia. Alizaliwa mwaka 1925 katika mji wa Hamedan, magharibi mwa Iran.
3492967