IQNA

Arbaeen 1446

Ayatullah Khamenei: Vita baina ya kambi za haki na batili daima vitaendelea

17:58 - August 25, 2024
Habari ID: 3479328
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema mbele ya wanafunzi wa vyuo vikuu katika maombolezo ya Arubaini ya Imam Husain AS kwamba mapambano baina ya kambi ya haki ya Imam Hussein (AS) na kambi ya batili ya Yazid kamwe havitomalizika.

Wanachuo kutoka kona zote za Iran, leo asubuhi wameonana na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa Tehran katika maombolezo ya Arubaini ya Imam Husain AS. 

Akizungumza katika kikao hicho, Ayatullah Khamenei amesema kuwa, kwenye ziara ya 'Ashura huwa tunasoma maneno yafuatayo: Mimi namwacha salama anayekuacheni salama na ninapigana vita na anayekupigeni vita, hivyo vita baina ya kambi ya Imam Husain AS na kambi ya Yazid kamwe haviwezi kumalizika (kwani ni vita baina ya haki na batili). 

ile vile amewashukuru vijana hao wa vyuo vikuu kwa kuendesha kumbukumbu hizo za Arubaini ya Imam Husain AS kwa njia bora akisema kuwa, Qur'ani imesomwa kwa namna nzuri kabisa, mashairi na Ziara ya Arubaini pia vimesomwa vizuri sana na kuongeza kuwa, mapambano haya baina ya haki na batili yataendelea.

Amekumbusha kuwa, katika safari yake ya kuelekea Karbala, Imam Husain AS alisema mara chungu nzima kwamba, hakutoka ila kwa ajili ya kupambana na dhulma, yaani ni vita vya kupigania haki dhidi ya batili, na vita baina ya kambi hizo mbili haviwezi kumalizika. 

Pia Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kisilamu amewaambia vijana hao wa vyuo vikuu kwamba ni wajibu waelewe jukumu lao na waisake na kuitafuta njia ya kutekeleza vizuri jukumu lao. Amesema, kukusanya mali na fedha hakupaswi kuwa ndilo lengo la maisha yao. Fedha, cheo, nguvu na nafasi ndani ya jamii ni vitu dhalili zaidi kufanywa kuwa ndilo lengo kuu la maisha ya mwanadamu. 

 
 

4233456

Habari zinazohusiana
captcha