Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei alihudhuria tukio hilo la kuondoa vumbi kwenye kaburi hilo takatifu ambalo liko Mashhad, kaskazini mashariki mwa Iran.
Tukio hilo pia lilihudhuriwa na Mfawidhi wa Haram ya Imam Ridha (AS) pamoja na wanazuoni kadhaa..
Wakati wa tukio hilo kulisomwa Ziyarat Jamia Kabirah na dua ya Aminallah.
Vile vile kulikuwa kasida na mashairi kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kufa shahidi Imam Hassan al-Askari (AS).
Kando ya tukio hilo, Kiongozi Muadhamu alitembelea pia kaburi la rais wa zamani wa Iran Ayatullah Seyed Ebrahim Raisi, ambaye aliuawa shahidi katika ajali ya helikopta mwezi Mei.
Imam Ridha (AS) ni Imam wa nane wa Waislamu wa madhehebu ya Shia, ambaye damu ni katika kizazi ya Mtume Muhammad (SAW). Ana hadhi maalumu miongoni mwa Wairani, kwani alitumia miaka yake ya mwisho ya maisha yake nchini Iran, mbali na mahali alipozaliwa katika Saudi Arabia ya kisasa.
Haram yake tukufu mamilioni ya wafanyaziara kutoka kote ulimwenguni mwaka mzima, haswa wakati wa hafla za kidini.
Raia wa Iran hutumia fursa yoyote inayojitokeza kutembelea na kuzuru Haram Takatifu ya Imam Ridha (AS).
4236241