Khayyam al-Zu'bi amebainisha kuwa katika barua hii Ayatullah Khamenei amesisitiza mshikamano wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na wanafunzi wa Marekani ambao wanakabiliwa na ukandamizaji wa polisi.
Amebainisha kuwa, nchi za Magharibi kwa miongo kadhaa zimeuunga mkono utawala wa Kizayuni, lakini jinai zinazofanywa na utawala ghasibu wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina zimekuwa kubwa kiasi kwamba hivi sasa watu wa Marekani na nchi za Ulaya wanaigeukia serikali zao na kupinga vita dhidi ya Ukanda wa Gaza. .
Katika miezi ya hivi karibuni, dunia imeshuhudia maandamano dhidi ya Israel katika vyuo vikuu vya Marekani, Canada, Uingereza, Ufaransa, Uholanzi na nchi nyingine, alisema.
Wanafunzi hao wametangaza kususia makampuni yanayoiunga mkono Israel na wanataka pia kukomeshwa kwa ushirikiano na vyuo vikuu vya utawala haramu wa Israel, al-Zu'bi alisema.
Ameongeza kuwa hivi sasa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amewaandikia barua wanafunzi hao, akitoa salamu za uungaji mkono wao kwa Wapalestina ambao wanatatizika kukomboa ardhi zao.
Barua hiyo pia inahusu uwezo wa Wapalestina katika kukabiliana na njama za Magharibi na Israel na kukabiliana na changamoto, mchambuzi huyo wa Syria aliendelea kusema.
Katika barua hiyo iliyotolewa siku ya Alkhamisi, Ayatullah Khamenei alipongeza maandamano ya wanafunzi wa vyuo vikuu vya Marekani ya kuunga mkono Palestina na Gaza katika miezi ya hivi karibuni, akisema wanasimama upande wa kulia wa historia, na amewanasihi kujitahidi kuifahamu Qur'ani.
3488593